Kampuni
ya filamu za Kibongo Kanumba The Great Films imeingia mzigoni kuandaa
filamu mpya iitwayo WONDER GIRL ikiwashirikisha waigizaji mahiri wa
tasnia hiyo.
Msanii mpya Lilian Mamuya na Rammy Galis
Wasanii walicheza kwenye filamu hiyo ni pamoja na Seth Bosco ambaye
ni mdogo wa marehemu Kanumba, Lilian Mamuya,Rammy Galis, Samofi, na
Keita.
Kampuni
ya Kanumba The Great Films kwasasa ina inaibua vipaji vipya katika
tasnia ya uigizaji,na kuwatambulisha wasanii wapya na wenye vipaji na
uwezo mkubwa kama vile Lilian Mamuya (kwenye picha juu) na Christina
Peter.
Zakayo Magulu akisoma scrip
Pia katika movie hii kuna watoto ambao wameonesha umahiri mkubwa
katika sanaa ya uigizaji hivyo inaashiria kua filamu hii ikitoka itakua
gumzo la jiji.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment