MSANII
filamu na muziki wa kizazi kipya wa Tanzania Baby Joseph Madaha maarufu
kwa jina la (Baby Madaha) amesema kwamba msanii mwenzake wa muziki
nchini,Naseeb Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platinumz si msanii bali
ni mfanyabiashara.
Madaha amesema kwamba
Diamond si mwanamuziki na kwamwe huwezi kumlinganisha na msanii kama
Barnaba Boy, anayefanya muziki kama sanaa na kazi kulingana na kipaji
chake na kwamba Diamond si msanii wa muziki bali ni msanii ngono
anayefanya biashara ya muziki kupitia mapenzi. 
Baby
madaha ambaye hivi sasa yuko nchini Kenya kwa shuguli za muziki amesema
kwamba, Diamond hajui kuimba na ndiyo maana amekuwa msanii wa matukio
huku nyota yake ikiegemea kwenye mapenzi na wasichana wenye majina
makubwa hususn wasanii.
Akizungumza na Mwanahabari katika mahojiano maalum leo baby Madaha alisema kwamba, "Binafsi niliposikia kwamba Diamond anaumiza kichwa kunasa penzi la msanii Elizabeth Michael maarufu kwa jina la (Lulu) sikushangaa hata kidogo. kwa sababu nilitambua kwamba soko lake la muziki limeanza kushuka hivyo lazima atafute eneo lingine la kujiimarisha kibiashara, ili jina lake liendelee kuwika".
"Siku wanawake maarufu nchini Tanzania watakapo jitambua na kuacha kulewa penzi la Diamond ndiyo itakayokuwa mwisho wa maisha yake kimuziki,kwa sababu hatakuwa na jipya na hivyo soko lake litaanza kuporomoka"alifafanua Baby Madaha.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment