Akiongea na mtandao wa Bongo5, Mr. Blue amesema kuwa sio yeye aliyechukua mkwanja wa promoter huyo bali naye aliambiwa kuna Mr. Blue fake anaetumia jina hilo kufanya utapeli.
“Sikuwa na show wala nini, ni waongo tu, kuna jamaa alinambia kuna mtu amemlipa hela kwa ajili ya kufanya show Kenya, ambaye anajiita Mr. Blue halafu hajatokea. Mimi nimewaambia wametapeliwa na watu wa kwenye mitandao, kama wana uhakika ni mimi waje wanikamate.” Alisema Kabayser.
“Unajua huwezi kufanya show nje ya nchi kama Kenya bila mkataba, kama wao wana mkataba na mimi nimechukua kiasi cha pesa kwa ajili ya pesa waanike hadharani watu waone.” Aliongeza.
Gazeti la The Star la Kenya liliandika kuwa Mr.Blue anatafutwa kwa kushindwa kutokea kwenye show aliyokuwa amesaini mkataba huko Mombasa, Kenya.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, Mratibu wa show hiyo, Sammy Ondwar Onyango, aliamua kushtaki polisi kwa sababu alidai kuwa alishamlipa msanii huyo kiasi cha shilingi 40,000 (za Kenya) kwa njia ya M-Pesa, na kwamba walikuwa wamekubaliana kiasi cha shilingi 100,000 (za Kenya) kwa show hiyo.
Promoter huyo alieleza kuwa hilo sio tukio la kwanza kufanyiwa hivyo na Mr. Blue kwani mwaka 2012 pia aliwahi kusumbuliwa na msanii huyo baada ya kumlipa pesa na kisha kuambiwa kuwa alichelewa basi kwa hiyo ikambidi promoter huyo kuzama mfukoni na kumpa nauli nyingine
0 MAONI YAKO:
Post a Comment