Wakati Dunia ikipinga vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake
na watoto hapa nchini Bado vitendo hivyo vimeonekana vikiendeleea ambapo
MTOTO Mmoja BENSON TOLE mwenye umri wa miaka Mitano mkazi wa Ruhuwiko
mjini Songea mkoani Ruvuma, amenusurika kifo baada ya kukatwakatwa kwa
kitu chenye ncha kali sehemu za usoni na Mzee mmoja LONGINUS HAULE
mwenye miaka 51 akimtuhumu mtoto huyo kumuibia matunda aina ya Mapera shambani kwake.
EMMANUEL MSIGWA kutoka mjini Songea
Mtoto BENSON TOLE kwa sasa amelazwa katika hospitali ya mkoa mjini Songea katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU), Madaktari wanaendelea kunusuru uhai wa mtoto huyu baada ya kupata mashambulio makali ya kucharangwacharangwa na kitu chenye ncha kali sehemu za usoni na mtuhumiwa mmoja LONGINUS HAULE mkazi wa Polisi Lizaboni mjini Songea.
Mzee HAULE anatuhumiwa baada ya kumfanyia unyama wa kutosha mtoto huyo na kisha kupoteza fahamu akimtuhumu kumuibia matunda aina ya mapera shambani kwake alimtupia kwenye nyumba moja ambayo haijaisha ujenzi wake akidhani tayari ameshamuua.

Afisa Muuguzi wa Hospitali ya mkoa mjini Songea, JOSEPH MTEWELE amesema
kwa sasa mtoto huyo yupo chini ya uangalizi maalumu na kwamba madaktari
wanaendelea na jitihada za kunusuru uhai wake kutokana na majeraha
makubwa aliyoyapata sehemu za kichwani.
Jeshi la polisi mkoani Ruvuma limetihibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba linaendelea kuchukua hatua zaidi za kumfikisha Mzee LONGINUS HAULE kwenye vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment