December 16, 2013

Mwimbaji wa kike wa bongo fleva Dayna Nyange ameelezea uamuzi wake wa kwenda Mwanza kufanya kazi na producer wa ‘One Love FX’ Tiddy Hotter, ikiwa ni miezi kadhaa imepita baada ya kutangaza kuwa atamtaja producer atakayefanya naye kazi baada ya kutofautiana na Sheddy Clever.
Dayna ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa aliamua kumfuata producer huyo jijini Mwanza kwa kuwa alihitaji kufanya kitu tofauti na kile kilichozoeleka kutoka kwake.
“Mi nilienda Mwanza kwa sababu nilikuwa namfuata Tiddy, na kukamilisha lengo la kile kitu ambacho nilikuwa nakihitaji tu, kwa sababu nilikuwa nataka kufanya kazi tofauti sana. Na kwa sababu nilikuwa nimeshaelewana na Tiddy nikaona sio mbaya, Mwanza sio mbali kama unataka kufanya kitu kizuri na kikubwa. Kwa hiyo ndiyo sababu ya msingi.” Amesema Dayna.
“Ni moja kati ya producers ambao ntafanya nao kazi kwa sababu nishafanya nae kazi na nimeshajuwa uwezo wake wa kufanya kazi kwa kuwa ameweza kunibadilisha kwenye huo wimbo wa MImi na Wewe.” Ameongeza.
Katika hatua nyingine, Mwimbaji huyo wa ‘Nivute Kwako’ amesema bado BASATA hawajampa mrejesho wa maamuzi ya malalamiko yake kuhusu kupokonywa mdundo wa wimbo wake na producer wake wa zamani Shedy Clever. Na kwamba kutokana na ukimya huo, ameamua kuendelea kufanya kazi zake

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE