December 17, 2013

mzee chifupa

Miaka 14 toka kuzaliwa kwa Clouds FM, The people station inawakumbuka baadhi ya Shujaa waliofanya vizuri na kuifikisha Clouds FM hapo ilipo ambapo moja kati ya watu hao ni Marehemu Amina Chifupa.

Mzee Chifupa alipata nafasi ya kuzungumzia Ushujaa wa Amina Chifupa kwa kusema ‘Ni kweli nyie mnamuenzi kama shujaa na sisi familia tunamuenzi kama shujaa kwa sababu katika vita aliyoingia nayo ya dawa za kulevya, sisi tulimuona kama shujaa hata kuna wakati flani watu waliniambia sasa huyu binti yako anazungumza hivi si wanaweza kumdhuru?? nikawambia mtu akidhurika kwa kutetea kundi fulani, kwa kutetea vijana, kwa kutetea wananchi, huyu amedhurika kwa kutetea wananchi na anakufa kama shujaa, na kweli Amina alikua shujaa’
‘Nahisi kuna mambo mengine nitayatoa kabla ya Decemeber kumalizika, ni mambo mazito nadhani yataishangaza dunia lakini yamezungumzwa, sisi tutatoa ushuhuda tu…. huwezi kuzuia ushuhuda wa mtu nafikiri kuna mambo tutayasema baadae ili watu wajue ushujaa wa Amina ulikuaje’

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE