Mwanamuziki wa Bongo Freva toka mkoani Morogoro Dayna Nyange ameandika ujumbe wake juu ya kifo cha mzee Nelson Mandela.
Katika AC yake ya Facebook Dayna ameandika
Katika AC yake ya Facebook Dayna ameandika
Tusiishie
kumlilia Mzee wetu Nelson Mandela bali tukae tukimuombea apumzike kwa
amaini, Tusimkumbuke kwa maneno bali tumkumbuke na kumuenzi kwa vitendo
vyake.Alihitaji wa Afrika kuwa hutru lakini hakung'ang'ania madaraka.
Alihitaji usawa kwa watu wote, hakuwa
mbaguzi kwa kipindi chake chote. Hakuwahi kujitenga na wengine. Alikuwa
radhi kumwaga damu yake kwa ajili ya wengine mfano pale alipotumikia
kifungo cha miaka 27 jela kwa ajili ya uhuru wa Afrika kisini. Ana mengi
sana ambayo hatuwezi kuyataja yote lakini Mandela ni mfano wa kuigwa.
Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment