Madole ambaye kwa sasa ni Meneja NMB Mt. Uluguru Br.
WACHEZAJI
wa klabu ya Morogoro Veteran wamempongeza Mwenyekiti wao, Hamis Madole
(Mboma) kwa kuhitimu shahada ya pili ya corporate managenment (MBA)
katikachuo kikuu cha Mzumbe huku wakimtaka kuongeza juhudi katika
utendaji kazi mkoani hapa.
Akizungumza na mwandishi wa habari
hizi katika mjini hapa kwa niaba ya wachezaji wenzake aisema kuwa
shahada ya pili aliyotunukiwa katika chuo kikuu cha Mzumbe anapaswa
kuongeza juhudi hasa katika utendaji kazi na kuleta ubunifu kutokana na
elimu hiyo.
Ally Bushiri alisema kuwa (Hamis Madole) ameongeza shahada ya pili na taasisi ambayo anafanyia kazi benki ya NMB ina changamoto kubwa hasa kwa kusaka mbinu mpya za kuwashawishi wateja ili kuweka fedha zao katika benki hiyo ambayo inahitaji mbinu mbadala ya kubuni wazo la ushawishi na kuwa kutokana na ushindani mkubwa uliopo ndani ya taasisi hizo za fedha hapa nchini
Naye Mwenyekiti huyo, Hamis Madole (Mboma) alisema ushauri huyo ataufanyia kazi na kujitahidi kubuni mbinu mbadala zitakazo wezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwemo zile zinazoimbuka taasisi hiyo hiyo ya fedha kwa kusaka wateja kuweka fedha katika benki hiyo.Wengine ni Mwenyekiti wa chama cha soka la wanawake mkoa wa Morogoro, Edna Lema, Detha Thomas aliyekipiga klabu ya Polisi Moro SC, Ally Shomari Reli Morogoro na Polisi Moro SC, Omari Mkesi Reli Morogoro na Victa Bundara, Yanga Sport Club, Mtibwa Sugar na Polisi Moro
0 MAONI YAKO:
Post a Comment