Moses Katabaro, Seif Ahmed
Mshambuliaji
wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel Okwi amewasili leo mchana
majira ya saa 9:45 katika uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyererer
akitokea nchini Uganda kwa shirika la ndege la Rwanda Air.
Okwi amekuja kujiunga na timu yake mpya Yanga SC
ambayo ataanza kuitumikia katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom
na mashindano ya Kimataifa.
Mara baada ya
kuwasili JK Nyerere Okwi alipokelewa na vipngozi wa kamati ya mashindano
sambamba na washabiki, wapenzi na wadau wa soka kwa ujumla.
Okwi
akiongea na waandishi wa habari uwanja wa ndege amesema anashukuru kwa
kufika salama jijini Dar es Salaam na hasa katika timu yake mpya ya
Yanga.
Kikubwa ameahidi kucheza kwa uwezo wake wote kuhakikisha anaisaidia timu yake mpya kufanya vizuri katika mashindano yote.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment