December 19, 2013

 
Leo ndio siku ambayo kampeni nzima ya ndoto za kitaa inazinduliwa rasmi ikiwa na dhumuni thabiti kabisa la kuhakikisha kuwa ndoto ya kijana wa kitanzania inapewa uhai na muongozo wa kuifanya iingie kwenye uhalisia na kubadilisha maisha sio tu ya kijana husika, bali pia jamii inayomzunguka na taifa kwa ujumla....
Tumekuwa tukipokea ndoto mbalimbali kutoka kwa watu mbali mbali, na bado tunaendelea kupokea mpaka itakapofika siku ya kesho ambayo ndio itakuwa siku ya mwisho ya kupokea ndoto zenu.....Hivyo kama una nia ya dhati ya kuiishi ndoto yako siku moja, bado hujachelewa.... tutumie kwa barua pepe kupitia email yetu ya ndotozakitaa@cloudstv.com
Au tuletee moja kwa moja hapa mjengoni, ofisi za Clouds Media Group Mikocheni
.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE