Mkutano wa Katibu Mkuu wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willbroad Slaa uliofanyika Uwanja
wa Kiganamo, Kasulu Mjini jana umevunjika baada ya polisi kupiga mabomu
ya machozi wakikabiliana na vijana waliorusha mawe kupinga mkutano
usiendelee. Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, vijana hao wanadaiwa
kuwa kati ya 10-15 ambao walirusha mawe baada ya wananchi kuwafukuza
wakitaka kuwapiga wakipinga kitendo chao cha kupiga kelele ili mkutano
usiendelee ndipo polisi walianza kulipua mabomu ya machozi na mkutano
kuvunjika.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment