Yaweza
kuwa ni nafasi ya wasanii wa Tanzania kujaribu upande wa pili wa maisha
yao kwenye utafutaji pesa manake msanii Kalapina toka block41 Kinondoni
Kikosi cha Mizinga ameamua kuangalia upande wa pili ambao ni masumbwi
a.k.a ngumi za kulipwa.
December
31 mkesha wa kuukaribisha mwaka 2014 umeingia kwenye headlines upande
wa Kalapina baada ya mpinzani aliyekuwa apigane nae usiku huo kutotokea
kwenye pambano hilo
Kalapina
anasema ‘mpinzani wangu alikuwepo na alipima siku ile lakini nafikiri
jina limemtisha na historia yangu ya mtaa imemtisha ameogopa na kweli
leo ningefanya mambo makubwa kwenye ulimwengu wa ngumi, ningeacha
historia nilijiandaa huyu mtu aondoke na machela’
‘kama
nilivyotangaza pale mapromota mi nipo tayari sasa hivi nipo tayari kufa
nipo tayari kupambana mi nimeingia kwenye ngumi rasmi sasa hivi,
kupigana ni sehemu ya maisha yangu na bondia atakayejitokeza kupigana na
mimi nitampigia saluti’ – Kalapina
Taarifa
ya kutokuwepo mpinzani wangu kwenye mpambano sikuwa nayo mapema hadi
napanda pale jukwaani nilikuwa na uhakika mpinzani wangu yupo na
tunapigana, mimi sibipiwi ukinibipu nakupigia…… taarifa hii imfikie’ –
Kalapina
Kwa
sasa hivi namtaka Japhet Kaseba namtaka na Mchumia Tumbo maana
wanaongeaongea sana hawa, kama Mchumia Tumbo anajifanya hana mpinzani
wakati wapinzani tupo’.
Kwenye hili pambano la Kalapina alitakiwa kuzichapa na Bahati
Mwafiyale ambae aliitwa mara kumi na hakutokea jukwaani hivyo Kalapina
akapewa ushindi aisee
Kwa hissani ya millardayo.com
0 MAONI YAKO:
Post a Comment