Moja kati ya tukio lililochukua vichwa vingi zaidi vya habari December mwaka jana ni kuhusu kukamatwa kwa mrembo wa Tanzania Jackie Cliff, na dawa za kulevya aina ya Heroin huko Macau, China.
Wengi wameizungumzia kwa mtazamo wao na wengine kama Mwanvita Makamba walituma ujumbe wao kwa wasichana wa kitanzania kuwashauri ili wasijikute katika balaa kama hilo.
Huddah Monroe wa Kenya naye alikuwa mmoja kati ya waliojitokeza hadharani na kuandika kwenye mitandao ya kijamii maoni yao kuhusu tukio hilo ambapo yeye alimponda kiaina Jackie Cliff kwa kumuita msichana mrembo aliyetaka maisha mazuri kwa haraka.
Mwimbaji wa ‘Nivute Kwako’ Dayna Nyange yeye amefunguka ya moyoni kupitia Instagram akiwakosoa wale wote wanaomsema vibaya Jackie Cliff na kumuona kama mkosefu sana. Na yeye amejikita zaidi kwa wanawake wenzake, hapa anaweza kuwemo Mwamvita Makamba na Huddah Monroe.
Lakini comments za baadhi ya watu wengine zilimuonya Dayna kuwa asipokubali watu wamkosoe vikali Jackie Cliff kwa alichokifanya wasichana wengine pia watafanya.
Dayna Nyange ameambatanisha picha za Jackie Cliff zinazoonesha akiwa amekamatwa, na kuandika:
Jamani Ivi ni nani kwenye USO huu wa dunia ambaye ajawai kukosea?????? Wapo binadamu wenzentu wanamakosa makuubwa Na hatuyajui na mengine yanajulikana.......
Kwanini tumekuwa mstali wa mbele kuwanyooshea watu vidole pale wanapokosea Tena Na kuwaombea Mabaya....... Dah!
Tukumbuke Sisi sote ni binadamu akuna anaejua kesho yake
Sina maana tutete uovu au kosa linapoafanyika Bali tutumie muda kutafakari kabla ya kumtuhumu MTU
Wanawake wenzangu huyu ni Mwanamke mwenzetu lakini sisi ndio tumekuwa mstari wa mbele kumlaani Na kutolea maneno mashafu Na hali Yukuwa tunajua hakuna alie mkamilifu
Binafsi imeniuma Na nimejiskia vibaya sana SAWA KAFANYA KOSA
Ila tusiwe majaji wa kutoa hukumu anza kujihukumu kwa maovu yako kabla ya kumuhukumu mwenzako
Tafakari maovu yako kabla kumnyooshea kidole mwenzako
TUACHE MAMLAKA ZA SHERIA ZIFANYE KAZI YAKE
Wanawake wenzangu TUPENDANE Natuwe na umoja Tushilikiane na tushauliana katika maamuzi yetu madogo Na makubwa labda tutaepuka ili tatizo
Inawezekana haya yote yanatokea kwetu sisi kwa kukosa ushilikiano Na upendo JACK DADA ANGU UMEKOSEA
Ila Sina sababu ya kukulaumu au kukuhukumu
wakati mwingine binaadamu ujifunza katokana Na makosa mungu ni wetu sote inshaallah atakusimamia.
Nimeshidwa kuvumilia nimeamua kusema nilichosema ila kama Kuna nilie mkwaza
naomba Aniwie radhi. MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU TUBARIKI WATANZANIA By Dayna nyange
0 MAONI YAKO:
Post a Comment