Kwa Matokeo haya yanaifanya Yanga SC iendelee kuongoza Ligi Kuu kwa kuwa mpaka sasa wana pointi 31 kwa kucheza mechi 14 wakifuatiwa na Azam FC wenye pointi 30.
Mechi ya leo hadi kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliyofanikiwa kuona kumfunga mwenzake,kipindi cha pili kilipoanza ilikua ni dakika sita tu Yanga walipata goli la kwanza lililofungwa na Didier Kavumbangu dakika ya 51, baada ya kupata pasi nzuri ya Simon Msuva.
Kwa Ashanti kupitia Mnigeria Bright Obinna walisawazishia dakika ya 60 baada ya kupokea pasi ya Hussein Swedi,Yanga ilipata bao lake la ushindi dakika ya 79 na lilifungwa na David Luhende kufuatia shuti kali alilopiga na kumfanya kipa wa Ashanti Daudi Mwasongwe kushindwa kuudaka
0 MAONI YAKO:
Post a Comment