Kuna
taarifa kuhusiana na baadhi ya Wabunge wa Ccm ambao wamesemekana kuwa
kwenye adhabu ambayo mfano wake ni kama kifungo cha nje kwenye Chama
Cha Mapinduzi.
Wabunge hao wanaosemekana ni wale walioonekana kuanza kutoa nia yao
ya kugombea urais hadharani kuwa ni pamoja na Mbunge wa Monduli Edward
Lowassa,Waziri Mkuu wa zamani Fredrick Sumaye na Mbunge wa Sengerema
William Ngeleja.
Kupitia kipindi cha Power Breakfast ya Clouds Fm Katibu wa Itifaki na
Uenezi wa Ccm Nape Nnauye amesema kuwa wabunge hao kwa sasa ‘Tafsiri
yake ni rahisi tunazo kanuni za usalama na maadili ya chama za mwaka
2010,ni za siku nyingi ila zimekua zikirekebishwa kila baada ya muda
fulani ili kukidhi mahitaji ya wakati’
‘Kanuni hizo zinatafsiri adhabu waliyopewa maana yake mtu anaepewa
adhabu hiyo atakua chini ya uangalizi wa chama kwa kipindi cha miezi 12
na inasema hivi Mwanachama aliyepewa adhabu ya onyo kali atakua katika
hali ya kuchunguzwa kwa muda usiopungua miezi 12 ili kumsaidia katika
jitihada zake za kujirekebisha’
‘Sasa katika kipindi cha uchunguzi yapo mambo mtu hatotakiwi
kufanya,kwa mfano ukiwa chini ya uchunguzi hutoruhusiwa kugombea
chochote katika kipindi hicho cha uchunguzi utatakiwa kusubiri hadi hiko
kipindi kiishe,tafsri ni kama kifungo cha nje ambacho unakuwa umebanwa
pengine hutakiwi kusafiri’
‘La pili ni kutofanya kosa la kimaadili kwa kipindi hicho endapo
ukifanya adhabu inaongezeka na ukimaliza kifungo kikaisha wanakwenda
kwenye kikao wanasema huyu mtu amejirekebisha sasa hivi yuko huru au
huyu
0 MAONI YAKO:
Post a Comment