Upigaji kura unaanza wiki hii katika vipengele 11 ambapo wananchi wenyewe watachagua majina ya washiriki watakaoshinda,awamu ya kwanza ya upigaji kura itafungwa baada ya wiki mbili kutoka siku ya kwanza ya upigaji kura na majina ya watu watano waliotajwa zaidi kutoka kwenye kila kipengele watachaguliwa kama watajwa wa mwisho.
Kuanzia hapo upigaji kura wa wananchi utajikita tu katika orodha ya majina hayo matano kwenye kila kipengele kinachoshindaniwa,Wiki moja baada ya majina ya washiriki kutangazwa, mchujo wa kwanza utafanyika katika kila kipengele na mtu mmoja ataondolewa.
Wiki moja baadaye mchujo wa pili utafanyika na kuwabakiza washiriki watatu kwenye kila kipengele ambao jumla watakua 33 wao watakuwa wageni wa heshima kwenye utoaji wa tuzo hizo.
Na tunzo hizi zitafanyika wiki moja baada ya mchujo huo wa mwisho katika hafla hiyo washindi watatangazwa na kila mshindi atapokea zawadi ya fedha taslimu ambazo ni T.shilingi 1,000,000 za Kitanzania pamoja na tuzo ya thamani
iliyotengenezwa kwa mkono kutoka kwenye mali ghafi asili za Kitanzania.
Tuzo za watu mwaka 2014 zitajumuisha vipengele 11 ambavyo ni pamoja na:
- MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW1 na jina’ kwenda
15678) -
KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW2 na jina’ kwenda
15678)
-
MTANGAZAJI WA TV ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW3 na jina’ kwenda 15678)
-
KIPINDI CHA TV KINACHOPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW4 na jina’ kwenda 15678)
-
MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW5 na jina’ kwenda 15678)
-
MWANAMUZIKI WA KIUME ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW6 na jina’ kwenda
15678)
-
MWANAMUZIKI WA KIKE ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW7 na jina’ kwenda
15678)
-
WIMBO UNAOPENDWA (2013) (tuma SMS yenye ‘TZW8 na jina’ kwenda 15678)
-
MUIGIZAJI WA FILAMU WA KIUME ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW9 na jina’
kwenda 15678)
-
MUIGIZAJI WA FILAMU WA KIKE ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW10 na
jina’ kwenda 15678)
- FILAMU INAYOPENDWA (2013) (tuma SMS yenye ‘TZW11 na jina’ kwenda 15678)kwa kutumia tovuti ya tuzo hizi ambayo ni www.tuzozetu.com ambapo utakutana na hatua rahisi
0 MAONI YAKO:
Post a Comment