Tuzo hizo zinaratibiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwa kushirikiana na TBL kupitia kinywaji chao cha Kilimanjaro.
Mratibu wa Tuzo hizo kwa upande wa Basata, Kurwijira Ng’oko
alisema mwaka huu wameboresha zaidi tuzo hizo, ambapo hivi sasa wanataka
muziki uwe ni ajira rasmi kwa hiyo msanii ambaye atapendekezwa katika
vipengele vya tuzo hizo kama hajasajiliwa Basata hataruhusiwa kushiriki.
Ng’oko alisema pia tuzo ya mtayarishaji chipukizi wa mwaka
haitakuwapo kwa vile watayarishaji ni wale wale kila mwaka na hivyo
kufanya tuzo kujirudia.
Naye meneja wa bia ya Kilimanjaro ambao ni wadhamini wa tuzo
hizo, George Kavishe alisema kuwa Watanzania ndio watakaoteua msanii
atakayeingia kwenye mchakato wa kinyang’anyiro cha tuzo hizo kwa kutoa
mapendekezo yao kwa njia ya simu au mitandao ya kijamii.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment