Yanga na Al Ahly ambao walichuana wikiendi iliyopita katika mchezo wa kwanza katika dimba la uwanja wa taifa Dar es Salaam, kwenye mchezo ambao uliisha kwa Yanga kushinda 1-0. Timu hizo zitarudiana jumapili wiki hii.
Hata hivyo habari nzuri kwa Yanga na mbaya kwa Al Ahly, ni kwamba mchezo huo hautokuwa na mashabiki kutoka na sababu za kiusalama.
Azmi Megahed, msemaji wa chama cha soka nchini Misri, amesema mashabiki hawatoruhusiwa kuhudhuria mechi hiyo kutoka sababu za kiusalama.
Jumamosi wiki iliyopita, polisi walipambana na mashabiki wa Zamalek White Knights ambao walijaribu kuingia katika uwanja wa Cairo kuangalia mchezo kati ya Zamalek dhidi ya mabingwa wa Angola Cabo Schrob. Fujo hizo zilipelekea kwa kukamatwa kwa mashabiki 33.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment