April 12, 2014


Ni mara ya kwanza kwa uke wa mwanamke kukuzwa katika maabara
Madaktari nchini Marekani wamefanikiwa kuwatengezea wanawake wanne sehemu ya uke kwa njia ya kisayansi.
Walitumia mfano wa seli ya uke na mifupa ya mwili kuweza kukuza uke huo katika maabara kwa kuzingatia wastani na umbo la kila mwanamke.
Baada ya matibabu hayo, wanawake hao wote inaarifiwa walielezea kupata hisia sawa na kamilifu,matamanio, kuridhishwa wakati wa tendo la ndoa pamoja na kutopata maumivu yoyote wakati wa tendo la ndoa.
Wataalamu walisema kuwa utafiti wao, ambao matokeo yake yalichapishwa katika jarida la kisayansi la Lancet, ni mfano wa hivi karibuni wa nguvu za mbinu tofauti na za kisasa za matibabu.
Wanawake hao walizaliwa na uke ambao haukuwa umeumbika vyema yaani ulikuwa na kasoro ya maumbile , tatizo linalojulikana kama ‘vaginal aplasia.’
Matibabu ya kisasa kwa tatizo kama hilo la kiafya yanaweza kuhusisha upasuaji ambapo ngozi au sehemu ya utumbo inatumika.
Celi zilichukuliwa kutoka kwa kizazi cha kila wanawake hao ambacho kilikuwa na kasoro ya maumbile na kukuzwa katika maabara ili kuweza kuzaana.
Picha za kizazi cha wanawake hao zilitumia kuwarekebishia uke wao.
Hili bila shaka ni jambo geni katika sayansi ya matibabu na pia inatoa taswira ya mambo yatakavyokuwa katika siku za usoni.
Jambo la Kutumia celi za mwili kubadilisha maisha ya wagonjwa tayari limefanyika na kuwasiaidia wagonjwa kupata kibofu cha mkojo, mishipa ya damu na koo.
Sasa unaweza kuongeza kwenye orodha hiyo, uke na pua.
Source: bbcswahili.com

Related Posts:

  • Umoja wa Ulaya wataka serikali ya Tanzania iwajibike   Umoja wa Ulaya (EU) umelaani kuongezeka kwa vitendo vya uvunjifu wa amani ukiwalenga wanasiasa na vitisho nchini Tanzania, na kutaka hatua kuchukuliwa mara moja kukomesha hali hiyo. Tamko lililotolewa Ijumaa… Read More
  • Official new Video: Salesale - Dayna Nyange      Audio ya wimbo huu wa Dayna Nyange, ilishatambulishwa tayari siku ya Alhamisi. Leo hii ametuletea Video ya wimbo wa Salesale. Video ipo katika ubora wa hali ya juu kabisa na inawezekana ikawa ni miungo… Read More
  • Zitto Kabwe akamatwa Morogoro, awekwa ndani   Kiongozi na mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo Ndugu zitto Kabwe, anashuikiliwa na jeshi la Polisi Mkoani Humo. Kwa mujibu wa taarifa za kichama kupitia ukurasa wa Twitte, Ndugu zitto amepelekwa … Read More
  • Brand New Audio: Alay - Nibebe  Mwanamuziki anayetamba kwa kuachia hit nyingi sana kwa sasa nchini tanzania Aslay, ametuletea wimbo wake mpya kabisa unaitwa Nibebe … Read More
  • Official Audio: Enock Bella _ Kurumbembe Mzee wa mbesi Enock Bella wa Yamoto Band, sasa kazi tu. Ameachia Rasmi wimbo wake wa Kurumbembe. Katika wimbo huu Enock anaonekana kufanya vizuri zaidi kutokana na mziki alioufanya utamfya kubadilisha style ya muziki wa … Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE