April 09, 2014


Mbunge wa Kawe (Chadema) Halima James Mdee na Mkurugenzi wa Jukwaa la Uchumi la Dunia kwa Bara la Afrika(WEF) Elsie Kanza, ni miongoni mwa viongozi wanawake 11 wa kisiasa kutoka barani Afrika waliotunukiwa tuzo ya kuwa viogozi wanawake wa juu wenye nguvu katika siasa.
Mdee ambaye pia ni Waziri kivuli wa Wizara ya Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi, aliunganishwa katika orodha ya wanawake jasiri katika masuala ya siasa barani Afrika kwa mwaka 2012.
Kwa mujibu wa kampuni ya Microsoft kutoka Marekani inayojihusisha na masuala ya Kompyuta iliyoandaa tuzo hizo, Mdee na Kanza ni miongoni mwa viongozi jasiri katika masula ya siasa kutoka barami Afrika ambao wanahitaji kupongezwa.
“Mwaka 2012 ulikuwa mwaka mzuri kwa viongozi wanawake wa kisiasa pamoja na marais wawili wanawake na viongozi wawili wanawake kutoka Umoja wa Afrika, Microsofti iliangalia wanawake 11 ambao wako makini katika masuala ya siasa barani Afrika,” ilieleza sehemu ya maelezo yaliyowekwa kwenye mtandao.
Wengine waliotunukiwa ni Rais wa Malawi, Joyce Banda; Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf; Mbunge kutoka Kenya, Charity Ngilu; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda, Louise Mushikiwabo na Waziri wake wa Afya, Agnes Binagwaho.
Wengine ni Rais wa Muungano wa Afrika, Nkosa Zana Dlamini Zuma; Waziri wa Fedha wa Nigeria, Ngozi Okojo-Iweala; Makamu wa Rais wa Zimbabwe, Joyce Mujuru na Mwenyekiti wa chama cha CPPG cha Ghana, Samia Nkhrumah.

ATOA SHUKRANI KUPITIA FACEBOOK
NAMSHUKURU SANA MUNGU KWA KUNIPATIA UJASIRI KAMA HUU WA KUWEZA KUWATUMIKIA WANANCHI WANGU, NA NASHUKURU SANA KWA KUPATA TUZO HII. NAOMBENI WANANCHI WANGU WOTE MNIOMBEE NIWEZE KUFANYA KAZI ZA TAIFA LETU KWA KADRI YA UWEZO WANGU, HUKU NIKISAIDIWA NA MWENYEZI MUNGU.
MUNGU IBARIKI AFRICA,
MUNGU IBARIKI TANZANIA.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE