April 14, 2014

Screen Shot 2014-04-14 at 2.40.34 PM 
Afrika Kusini ni nchi yenye uchumi mkubwa Afrika ambao umevutia Waafrika wengi kukimbilia huko kwa ajili ya kufanya kazi kama za Udereva, uuzaji mafuta kwenye vituo vya mafuta pamoja na kazi nyingine mbalimbali.
Taarifa kutoka kwenye mji wa Pretoria ni kwamba Watanzania ambao wanamiliki na kufanya biashara mbalimbali zikiwemo za Maduka na wale wanaomiliki hoteli, wamevamiwa wakiwa kwenye mali zao na kufanyiwa uharibifu na nyingine kuchomwa moto.
Ni kundi la watu ambalo linaendeleza uvamizi huu ambapo linawashutumu Watanzania hawa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya, yani kwa ufupi Watanzania wanasema hata kama kweli wangekua wanafanya hii biashara, walio na mamlaka ya kuwavamia ni Polisi na sio hao raia.
Screen Shot 2014-04-14 at 2.40.25 PM 
Inaaminika kundi hili lina sehemu kubwa ya madereva Taxi wazawa wa nchi hiyo ambao wamekua wakiumizwa na jitihada za raia wa kigeni wa Nigeria na Watanzania ambao wamejazana kwenye mtaa wao wakimiliki maduka mbalimbali yakiwemo ya nguo pamoja na hoteli.
Tayari balozi wa Tanzania amekutana na Watanzania hao na kuahidi kulifatilia ambapo ni Watanzania watano wamejeruhiwa wakiwemo watatu ambao bado wako hospitali na mmoja wao kavunjika mkono, mmoja kapigwa kichwani.
Kabla ya Watanzania wengine kuwahi kufunga maduka yao, maduka matatu ya Watanzania pamoja na hoteli mbili zinazomilikiwa na Watanzania zilivamiwa na wakachuchukuliwa simu na watu kupigwa ambapo polisi walipokuja hakuna chochote kilichofanyika zaidi ya maelezo.
Picha hizi zote zilipigwa na Mtanzania akiwa anakimbia baada ya kufanikiwa kufunga duka lake.
Source: Millardayo.com

Related Posts:

  • Afisa wa chanjo ya Polio auawa   Afisa wa idara ya afya nchini Pakistan aliyekuwa akisimamia kampeini ya kutoa chanjo ya kupambana na maradhi ya polio maeneoya vijijini karibu na mpaka na Afghanistan ameuawa kwa kupigwa risasi. Bwana Akhtar K… Read More
  • CUF: "Tutatoa muelekeo hatma ya kisiasa Zanzibar" Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Magdalane Sakaya   Chama cha Wananchi (CUF), kimesema kinajiandaa kutoa tamko zito kuhusu hatima yake kisiasa visiwani Zanzibar. Kufuatia hatua ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguz… Read More
  • Rais Magufuli aibarikia Taifa Stars Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameitakia heri timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) katika mchezo wake dhidi ya Timu ya Taifa ya Chad, utakaofanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Da… Read More
  • Rais Magufuli ahudhulia ibada ya Pasaka Azania KKT Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Alex Malasusa alipowasili kwa Ibada ya… Read More
  • Bad News:Golikipa wa Simba afariki Dunia Aliyekuwa Golikipa wa zamani wa Simba, Abel Dhaira amefariki Dunia   Abel Dhaira amefariki dunia leo nchini Iceland alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa kansa ya utumbo. Golikipa huyo aliyekuwa na miaka 2… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE