
Aibu nzito! Msanii chipukizi wa Bongo Fleva, Venas John Bebu ‘Bebuz’
amenaswa laivu akivunja amri ya sita (kuzini) na mwanafunzi wa sekondari
ufukweni. Tukio hilo la aibu lilijiri wiki iliyopita mishale ya saa
8:00 usiku kwenye Ufukwe wa Coco, Dar ambapo polisi jamii walimnasa
jamaa huyo aliyedaiwa ni swahiba mkubwa wa mwanamuziki, Abdul Sykes
‘Dully Sykes’ ambao hivi karibuni walitoa kibao kipya kijulikanacho kwa
jina la Bunyerobunyero.
Mara baada ya kunaswa, Bebuz alianzisha varangati kubwa lakini polisi
jamii walimtuliza kwa virungu kisha kumfunga pingu na kumtaka atulize
mzuka atoe ushirikiano vinginevyo angeumia.
Kijana huyo alitulia kwa muda lakini alipowaona OFM wakipiga picha,
alilianzisha tena na kutaka kuvunja kamera huku akitamba kuwa alikuwa na
uwezo huo ,Hata hivyo, OFM walikuwa makini kama kawaida yao.
Ufukwe wa Coco umekuwa ukilalamikiwa kwamba hukutanisha watu wenye
malengo mbalimbali lakini wanaokwenda kwa ajili ya kufanya ufuska usiku
ni wengi hasa siku za wikiendi ambako kunakuwa na burudani ya disko.
Kikosi maalum cha kufichua maovu OFM (Opereshen Fichua Maovu) cha
GlobalPublishers kilipiga kambi katika ufukwe huo kwa muda wa wiki moja
na kushuhudia maovu yanavyofanyika.
Pia OFM ilibaini kuwa katika ufukwe huo kumekuwa kukifanyika vitendo
ambavyo siyo vya kiustaharabu ambapo watu wamekuwa wakifanya ngono
katika vichaka na kwenye maji.
Katika siku za hivi karibu, machangudoa wamekuwa wengi ufukweni hapo na
baadhi yao ni vibaka ambao wamekuwa wakitoka nduki na nguo za wanaume
huku wakisachi na kuchukua kila kitu
0 MAONI YAKO:
Post a Comment