May 06, 2014

 
 Hapa akijifanya kusoma huku akificha sura yake
 
 Baada ya kuona mafrashi yanazidi kummulika aliinua uso na kusema "Shekidele achana na ishu hizo" baada ya kusema hivyo aliangua kicheko
 Hapa akiwa na mchezaji wa zamani wa polisi Moro Mbaraka Masenga
 
 Kaseja mwisho mwenye kofia nyekundu akishiriki kozi hiyo
 
 Akizidi kuficgha sura
       Mkufunzi wa kozi hiyo Alphonsi Magari.
    KIPA namba moja wa timu ya Taifa ya Tanzania'Taifa Stars na klabu ya Yanga Juma Kasema muda huu amenaswa na Mtandao huu akishiriki Kozi ya mafunzo ya ukocha wa mpira wa Miguu inayoffanyika kwa sasa katika moja ya darasa la Shule ya Msingi Bungo iliyopo Manispaa ya Morogoro.

Kozi hiyo ya wiki moja inaongozwa na mkufunzi Alphoni Magari ambapo katika hali ya kushganga Kaseja baada ya kumuona  mpiga picha hizi aliacha kusoma na kuamu kuficha sura yake akikwepa kupigwa picha jambo lililowashnga washiriki wenzake.

Hata hivyo licha ya Kaseja kuficha sura yake mpiga pichawetu aliendele kumfotoa picha  nyingi jambo lililomfanya kipa huyo kuhamaki na kumtaja jina Mwandishi huyo akimsihi asiendelee kumpiga picha.

Baada ya ligi kuu Tanzani bara kumaliziki hivi karibuni kwa Azam kuibuka Mabingwa na yanga iliyokuwa akishikilia ubingwa huo kuambulia nafasi ya pili wachezaji wengi kwa sasa wako mapunziko mikoani.

lkumbukwe Kaseja ambaye baada ya kutoka kwao Kigoma alisajiriwa na Reli ya Morogoro,baadae akijiunga na Mtibwa kabla ya kutimkia Simba na sasa yuko yanga.

Kwa kipindi alichoishi Morogoro Kaseja alifanikiwa kujenga nyumba iliyopo Kihonda maghorofani ambapo nyumba yake iko mtaa mmoja na nyumba za wachezaji wenzake Ulimboka Mwakingwe,Jumanne Tondolo'Shengo' na kocha mkuu wa Mtibwa Sugar Mecky Mexime.

Hivyo baada ya ligi hiyo kufika tamani Kaseja yuko mkoani hapa kwa mapunzi na kwamba baada ya kusikia uwepo wa kozi hiyo ameamu kujiunga kwa lengo la kuongeza taaruma yake hiyo ya ukocha.

Kwa sasa Kaseja licha ya kuwa mchezaji wa yanga na timu ya taifa ameteuliwa na TFF kuwa kocha wa makipa wa timu ya taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 ambayo hivi karibuni imefanikiwa kusonga mbele katika mashindano ya Afrika kwa vijana wenye umri huo baada ya kuwatoa wenzao wa kenya
 
Kwa hisani ya Dastan Shekidele

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE