Mwanamke huyo alikumbwa na adha hiyo juzi saa nne usiku nyumbani
kwake na hadi jana, saa nne asubuhi baadhi ya vipande vya nyama vya
sehemu za siri na chini ya tumbo, jirani na kitovu, vilikuwa bado vipo
katika eneo la tukio.
Ofisa Habari wa Hospitali ya Tumbi, Kibaha, Gerald Chami alisema jana
kwamba kutokana na majeraha aliyokuwa nayo alipelekwa katika chumba cha
upasuaji kushonwa.
Chami alisema majeruhi huyo ambaye alikuwa akizungumza kwa tabu
alisimulia kwamba siku moja kabla ya tukio, mumewe alimkuta akiongea na
simu ya mkononi na alimnyang’anya na kuisikiliza na alipobaini kuwa ni
sauti ya mwanamume hakuuliza kitu, bali alimrudishia simu na kuondoka.
Alisema muda mfupi baadaye alirudi akionyesha dalili za kuwa na
hasira na ndipo mama huyo alipomhoji mumewe juu ya hatua yake ya
kumnyang’anya simu na kumuuliza ilikuwa na shida gani. Hatua hiyo
ilisababisha ugomvi mkubwa.
Chami alisema mwanamke huyo alimwambia kuwa baada ya ugomvi huo,
aliamua kuondoka nyumbani hapo na kwenda kwa ndugu yake jirani lakini
muda mfupi baadaye, mume wake alimfuata na kumlazimisha kurudi nyumbani
lakini alimkatalia na kumtaka wazungumze ugomvi wao hapohapo ili wapate
suluhu.
“Huyu mama alisema katika ubishi
huo wa wapi wakajadili ugomvi wao huo, ndipo ndugu zake wakamshauri
kuwa kwa vile mumewe alitaka wakayamalize kwao basi aende.
Hata hivyo, walipofika nyumbani badala ya kujadili ugomvi, alianzisha
tena ugomvi na kisha kuchukua kisu na kumtishia kumchinja na katika
patashika hiyo, Chami alisema mama huyo alimweleza kwamba aliishiwa
nguvu na kuanguka ndipo mwanamume huyo alipomjeruhi vibaya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei alisema licha ya kwamba
mgonjwa huyo huko Tumbi, asingeweza kuzungumzia suala hilo kwa kuwa
lilitokea katika Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment