May 03, 2014


Ilikuwa ni safari ya kawaida ambayo ilitarajiwa kuwapa faraja watoto. Lakini hali imekuwa tofauti baada ya matarajio hayo kugeuka majonzi kwa mtaa mzima kutokana na kuondokewa na watoto watatu kwa wakati mmoja.

Ni mara chache sana watoto hutoka pamoja kwenda mbali kufurahia na wenzao. Hivyo Janet, Ndimbumi na Eva waliamini kuwa siku hiyo ingewapa furaha na pengine hadithi za kwenda kusimulia shuleni, lakini haikutokea kama walivyotarajia; simulizi zikawa tofauti.

“Tulistuka kuuona mwili wa Janeth ukiwa unaelea juu ya maji,” anasema kaka yake, Goodluck Kihoko (14) ambaye siku hiyo alienda pamoja na watoto wengine 20 kwenye Hoteli ya Landmark iliyo Mbezi Beach, jijini Dar es salaam.

“Tuliwaita walinzi, lakini wakapuuza. Tuliwaita walinzi kwa muda mrefu ndipo wakafika na wakati huo mama na wale vijana walikuwa mbali na pale tulipokuwa tukiogelea. Baada ya muda walikuja na tukauona mwili wa pili ukiibuka,” anasimulia Gooluck kwa uchungu.

Wakisimulia tulio hilo, watoto waliokuwa katika msafara huo Florian Masonda (12) anasema  walichukuliwa na jirani yao, Anita Mboka kwenda kusherehekea nao siku ya kuzaliwa kwa mtoto wake, Derick Mboka aliyekuwa anatimiza umri wa mwaka mmoja.

Florian anasema baada ya kufika hotelini hapo walianza kucheza mpira wa kikapu huku watoto wengine wakiogelea na mama Mboka aliyewapeleka pamoja na wale vijana wakiwa wamekaa wakipata vinywaji.

“Tulikuwa tunacheza mpira wa kikapu na ghafla tulisikia kelele baada ya mtoto mmoja kuja kutuita na kutupatia taarifa kuwa kuna watoto wamezama chini ya maji na hawaonekani. Tuliondoka na baada ya kufika kwenye bwawa la kuogelea ndipo tulipowaona wakiwa tayari wamekunywa maji mengi,” anasema Florian.

Naye Goodluck anasema yeye na watoto wenzake zaidi ya 20 waliondoka Kijitonyama wakiwa na vijana wanne kwenda kwenye sherehe hiyo.

“Tuliondoka hapa saa kumi na moja jioni, baada ya kufika kule tulianza kuogelea kwenye bwawa. Watoto wengine walikuwa wanakwenda kuogelea kwenye maji marefu, walizuiliwa mara tatu, lakini baada ya walinzi kuondoka walirudi na kuzama,” anasema.

Kwa uchungu alionao Bahati Sisala alikuwa amekaa akiwa ameduwaa macho yake yamevimba na mekundu kutokana na machozi yaliyomtoka kwa muda mrefu.

Akiwa amejiinamia bado haamini mkasa uliomkuta binti yake kipenzi Ndimbumi Sisala (9) uliosababisha kifo chake ambacho kilimkuta ghafla katika hoteli hiyo Aprili 27.

Lugano Mwakyosi, ambaye ni msemaji wa familia hiyo inayoishi Kijitonyama Mpakani A, anasema Sisala amechanganyikiwa kutokana na kifo cha binti yake aliyempenda sana.

Related Posts:

  • Wakulima Morogoro waandamana   Zaidi ya wakulima 80 wa eneo la Mguluwandege na Lukobe kata ya Kihonda manispaa ya Morogoro wameandamana kwa lengo la kuhamishia makazi katika ofisi za ardhi manispaa ya Morogoro wakishinikiza mkurugenzi … Read More
  • New Audio: Aloma- Tutoke Huu ni wimbo mpya kutoka kwa msanii Aloma toka mkoani Morogoro. Wimbo umefanyika Storm Music chini ya Producer B5 mkoani Morogoro Waweza kuuskiliza hapa chini … Read More
  • Ghasia za ubaguzi zapingwa Afrika Kusini   aelfu ya raia katika mji wa mashariki wa Durban nchini Afrika Kusini wanaandamana kupinga ghasia za hivi majuzi dhidi ya wageni. Takriban watu watano wameuawa tangu wiki iliopita katika ghasia dhidi ya wahamiaji am… Read More
  • Mpya ya Bushoke hii hapa -Nimekumanya   Baada ya kukaa mimya kwa muda mrefu, hatimaye mkali wa nyimbo kama, barua, Mume bwege na nyimbo nyingi zilizo hit Bushoke, ameamua kuja na ngoma yake hii mpya kabisa. … Read More
  • ACT - Wazalendo waiteka Morogoro, Zitto kabwe akabidhi chama   Zitto Kabwe akihutubia Mkutano Morogoro  Wakazi wa Mkoa wa Morogoro na vitongoji vyake leo hii kwa mara ya kwanza wamekipokea Chama kipya cha Wazalendo cha ACT chini ya kiongozi mkuu wa chama hicho  Zitt… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE