May 02, 2014

Waandamanaji nchini Nigeria wakidai wasichana waliotekwa katika mji wa Chibok, Borno warejeshwe
Polisi nchini Nigeria wamewataka wazazi wa wanafunzi wasichana zaidi ya 200 waliotekwa kuwasilisha picha za mabinti hao.
Wasichana hao walichukuliwa na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Kiislam kutoka shuleni kwao katika jimbo la Borno zaidi ya wiki mbili zilizopita.
Polisi wa jimbo la Borno wameiambia BBC kuwa serikali inataka kuthibitisha bayana ni nani ambaye ametoweka kwa sababu vitabu vya kumbukumbu vya shule vilichomwa moto katika shambulio hilo.
Waandamanaji wengine wakitaka rais wa Nigeria asaidie kuwaokoa wasichana waliotekwa jimbo la Borno
Polisi wamesema kwa sasa inafikiriwa kuwa wasichana wapatao 223 bado hawajulikani walipo.
Maandamano yalifanyika siku ya wafanyakazi duniani Mei Mosi, ambayo ni mapumziko, waandamanaji wakitaka hatua zaidi zichukuliwe kuwaokoa wanafunzi hao wa kike.
Kundi la Kiislam la Boko Haram halijatamka lolote kuhusiana na tuhuma zinazolikabili kuwa wapiganaji wake wamehusika na utekaji wa wanafunzi hao kutoka shuleni kwao katika mji wa Chibok usiku wa manane wa tarehe 14 Aprili 2014.
Kundi hilo, ambalo jina lake lina maana ya "Elimu ya mgaharibi ni haramu" katika lugha ya Kihausa, limekuwa likiendesha mashambulio mbalimbali kaskazini mwa Nigeria katika miaka ya hivi karibuni, huku watu 1,500 wakikadiriwa kuuawa katika ghasia hizo na msako wa vyombo vya usalama mwaka huu pekee.

Related Posts:

  • JAHAZI YATISHA USIKU WA VALENTINE DAR LIVE   Nyomi ya wapendanao ikifuatilia kwa makini burudani. Zawadi za Valentine zikiuzwa ndani ya Darlive kama zilivyonaswa na kamera yetu.   Dada huyu alishindwa kujizuia kuyarudi.   Tx Moshi Juniour akim… Read More
  • NEW AUDIO : ALBERT MANGWEA ft MIRROR - ALMA   Ni wimbo mpya kabisa toka kwa marehemu Albert Mangwea. Moja  ya kazi alizowahi kuzifanya  na hazijatoka ni pamoja na hii Brand new "ALMA" akiwa na Mirror, iliyotambulishwa leo hii na mama yake mzazi … Read More
  • AKINA DADA MNAOJIONA WAZURI HII INAWAHUSU SANA Ukijaliwa kuwa Msichana mzuri na  mrembo,usidhani utatetemesha kila Mwanaume,kuna wanaume na akili  zao kichwani,urembo wako hauwasumbui,kama bichwa lako nikanyaboya,uzuri wako hausaidii kitu,na utasha… Read More
  • FAMILIA YA MANGWEA YAAMUA KUKUSANYA NYIMBO ZAKE   Albert Mangwea ni miongoni mwa wasanii wanaoaminika kuwa na nyimbo nyingi sana ambazo bado hazijatoka,wakati wa kumbukumbu ya kifo cha Mangwea Morogoro iliyofanyika November 2013 Millardayo.com iliongea na f… Read More
  • MASOGANGE AAMUA KUFUNGUKA VIDEO Queen matata Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ amewajia juu kundi kubwa la wanaume linalomtaka kimapenzi wakati wanatambua vyema kuwa ana mtu wake. Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Masoga… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE