
Mbunge wa Kigoma Mh Ziito Kabwe amekabithiwa cheo na umoja wa kamati za mahesabu ya serikali ya nchi za SADC (SADCOPAC)
Zitto amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa umoja wa kamati za mahesabu za
nchi za Africa kuziba nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Msumbiji.
Ni
dhahiri mapambano dhidi ya ufisadi katika bara la Afrika yatafanikiwa
iwapo mabunge ya wananchi yanasimamia vema serikali. Ni heshima kubwa
kwa nchi yangu kupata fursa hii ya kujenga utamaduni wa uwajibikaji
kupitia kamati za BUNGE za mahesabu. Ni changamoto kubwa ninayoipokea
kwa unyenyekevu mkubwa. Kuwa Katibu Mkuu wa AFROPAC ni fursa ya kujitoa
kujenga Afrika Mpya yenye kujali rasilimali za umma kama Mali ya
wananchi. Mungu atanilinda na kunisaidia katika kutimiza wajibu huu.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment