May 11, 2014


Muigizaji mashuhuri wa Hollywood nchini Marekani, Shailene Woodley, mapema wiki hii aliwashangaza watu alipofichua kuwa yeye hula udongo kila siku kwa kupima kijiko kimoja.
         
Lakini je ni sawa kula udongo kwa sababu za kiafya?
Muigizaji huyo, aliyewahi kucheza filamu mashuhuri ya Descendants akishirikiana na George Clooney, alisema kuwa udongo ni moja ya vitu vyenye afya kwa mwili ambavyo yeye mwenyewe anaweza kula.
“nimegundua kuwa udongo unaweza kukupa afya nzuri mwilini. Najua wengi wanadhani kuwa mimi ni kichaa ninaposema kwmaba , udongo una uwezo wa kusaidia kusafisha mwili wako kutokana na madini mazito mwilini,” alisema Woodley.
Anasema alijifunza kula udongo kutoka kwa dereva mmoja mwafrika. Baadhi ya marafiki zake hutengeza dawa ya kusugua meno kutoka kwa udongo ambao unaweza kumeza. Hata hivyo alisema ni muhimu kuwa udongo huo kabla ya kuliwa uwe safi.
Tabia ya kula mchanga au udongo inajulikana kwa kiingereza kama Geophagy.
Shailene Woodley
Ni jambo la kawaida watu kula udongo Afrika au Mashariki ya kati ingawa sharti uwe yametengezwa kwa mfano wa tembe. Hii ni kwa mujibu wa mtaalamu wa afya katika hospitali ya Kings College, London, Rick Wilson.
Sababu muhimu ambayo inaweza kukufanya kula udongo ni kukosa madini ya ZINC mwilini, lakini wataalamu wanasema kukosa madini hayo mwilini sio hatari na kwamba sio jambo la kawaida barani Afrika watu kukosa sana madini hayo mwilini.
Lakini Shailene Woodley anaamini kuwa kula udongo inaweza kukupa afya nzuri.
Udongo hata unaweza kuathiri mwili wako hasa ikiwa una chembechembe za Arsenic au Lead.
Wanawake wajawazito wakati mwingine hupata hamu ya kula udongo au mkaa kwa kukosa madini fulani mwilini,anasema daktari Sartah Jarvis.
Na inaweza kueleweka ikiwa ni barani Afrika kwa sababu ya changamoto ya lishe bora lakini kula tu udongo kwa sababu ya kupenda , hiyo haiwezekani.

Related Posts:

  • Yanga SC yatangaza kuanza na Tv kisha Radio   Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kuanzisha vipindi vya michezo vitakavyo ruka katika luninga ya Azam TV kama ilivyo kwa mahasimu wao Simba SC ambao wao tayari walishaanza pamoja na timu ya Azam FC. Wakio… Read More
  • Simba Yang'oka kiume Misri Baada ya wekundu wa msimbazi Simba kutolewa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika na timu ya Al Masry huku wakitoka sare ya 0 – 0 nchini Misri, afisa habari wa klabu hiyo, Haji Manara amesema kuwa tim… Read More
  • About Life, Na Peace Ze prezdaa Machaku Media, tunakukutanisha na mtangazaji wa kipindi cha Planet Base cha Planet Fm ya Morogoro. Jamaa anaitwa Peace Ze Prezdaa. Hapa licha ya kufanya kipindi cha kiburudani katika radiko, lakini hapa anajaribu kuzungu… Read More
  • Rihanna awauliza mashabiki wake kufuta Snapchat baada ya ...   Last Week End Snapchat got into some serious polemic with it last controversial compaign including Chris Brown and Rihanna. “Would you rather slap Rihanna” or “Punch Chris Brown ?”. Snapchat last ad seriously p… Read More
  • Yanga Yaangamia Botswana Yanga SC yaangukia katika michuano ya kombe la Shirikisho baada ya kutolewa klabu bingwa Barani Afrika dhidi ya Township Rollers FC huko nchini Botswana. Yanga SC imeyaaga mashindano hayo baada ya kulazimishwa sare ya … Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE