
Wakati
jana mumewe Emmanuel Mbasha (32) akipandishwa kizimbani kwa mara ya
pili kwa soo la ubakaji wa shemejiye, mwimba Injili kinara Bongo, Flora
Mbasha (31) amepitia katika hatua tatu za aibu.
Mbasha
ambaye naye ni mwimba Injili na mfanyabiashara alitarajiwa kupandishwa
kizimbani jana kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Ilala, Dar
akitokea mahabusu Keko akikabiliwa na mashtaka mawili ya ubakaji wa
shemejiye mwenye umri wa miaka 17.
Habari
kutoka kwa mtu wa karibu wa Flora ambaye alihama nyumbani na kwenda
kuishi hotelini maeneo ya Sinza, Dar, kitendo hicho kilimuingiza staa
huyo kwenye hatua ya tatu ya aibu na kujikuta akiwa katika masikitiko
makubwa.
AIBU YA KWANZA
Kwa mujibu wa mtu huyo wa karibu aliyeomba hifadhi ya jina, aibu ya
kwanza inayomuuma Flora ni ile ya ndoa yake kuingia kwenye gogoro kisha
kudaiwa kutengana na mumewe kinyume na kile anachokihubiri kupitia
nyimbo zake zinazopendwa na wengi ndani na nje ya Bongo.
“Unajua lile neno la ‘mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, bali
mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe’ (Mithali 14:1) linamfanya
awe na aibu mbele za watu.
“Unaambiwa kanisani (anasali Kanisa la Ufufuo na Uzima la Mchungaji
Josephat Gwajima kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Dar) anaona aibu
hasa kwa waumini wenzake.
“Flora amedumu na Ima (Mbasha) kwenye ndoa kwa miaka 12 hivyo kutokea
kwa kilichotokea ni aibu kwani tayari walikuwa wamekomaa tofauti na
walipoona wakiwa na umri mdogo.
“Hebu fikiria, mtoto amekuwa mkubwa, anaposikia mama ana matatizo na
baba si ni aibu jamani? Cha msingi tuwaombee wamalize matatizo yao,
inaweza kusaidia kuifuta aibu hiyo kwani imeandikwa ‘Ndoa na iheshimiwe
na watu wote…’ ( Waebrania 13 : 4 -),” alisema mnyetishaji wetu
akisisitiza kuwa akitajwa ataonekana mvujishaji wa mambo ya siri ya
wanandoa hao.
AIBU YA PILI
Chanzo hicho kiliendelea kutiririka kuwa aibu ya pili inayomkabili Flora
ni skendo ya yeye kudaiwa kuhamishia makazi kwa mchungaji wake,
Gwajima.
Katika aibu hiyo, mumewe alinukuliwa na gazeti la Uwazi akimlalamikia
mchungaji huyo amwachie mkewe kwani yeye ndiye alisababisha sakarakasi
zote hizo za ndoa yake.
Ilidaiwa kuwa kwa mke wa mtu achilia mbali mhubiri kwa njia ya nyimbo, kitendo cha kukumbwa na skendo nayo ni aibu pia.
“Kwa mtumishi kutajwa kwenye jambo kama hilo lisilo na mrengo wa
kupendeza masikioni mwa watu, ni aibu kuu,” kilidai chanzo hicho.
AIBU KUU YA TATU
Ilisemekana kuwa achilia mbali ndoa, mambo ya mchepuko lakini aibu kuu
ya tatu kwa Flora, ni kashfa ya ubakaji wa shemejiye inayomkabili mumewe
Mbasha.
“Unajua usifikirie kwamba mume akipata aibu mke anaweza kuikwepa. Hawezi
kwa sababu ‘wanazungumza lugha moja’ (yaani ni mwili mmoja). Ona sasa
mume anapandishwa kizimbani kwa ubakaji.
“Pia usifikiri watu watasema kashfa ni ya Ima peke yake. Kwanza hata
kutamka watu wanasema mume wa Flora. Ikumbukwe aibu ya mume ni ya mke
pia. Ni vigumu mno kwa Flora kusema aibu ni ya mumewe pekee,”
alitiririka mto habari huyo.
FAMILIA ZATOFAUTIANA
Wakati hayo yakiendelea, habari zinadai kuwa familia za pande zote zinatofautiana huku kila moja ikilaumu nyingine.
Ilidaiwa kuwa upande wa Mbasha unamlalamikia mama wa Flora kuwa
anamuunga mkono mwanaye badala ya kusaidia kutuliza hali ya hewa.
Ilielezwa kuwa upande wa Flora wao wanamlaumu Mbasha kwa madai kuwa
chanzo cha yote ni mgawanyo wa mali hasa baada ya kuona kuwa hakuna tena
ndoa.
FLORA ANASEMAJE?
Akizungumza na Ijumaa
juzi kwa njia ya simu, Flora alitoa la moyoni: “Kweli naumia sana tena
sana. Kwa sasa kesi ipo mahakamani, siwezi kuizungumzia lakini ndiyo
hivyo. Siyo siri nateseka sana.”
Mbasha anadaiwa kumbaka
ndugu wa Flora ambaye ni yatima kati ya Mei 23 na 25, mwaka huu ambapo
kesi yake inaendelea kuunguruma baada ya kukaa mahabusu ya Keko kwa siku
kadhaa ambapo sheria ndiyo itakayoanika siri zote juu ya sakata hilo.
Crediti: GPL
0 MAONI YAKO:
Post a Comment