June 06, 2014

Msanii Madee akichat Live leo katika ukurasa wa Facebook wa EATV 
 
   Rais wa Manzese ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya tema mate tuwachape Madee amefunguka na kusema kuwa anampenda na kumkubali Ney wa mitego kutokana na ukweli kwamba mkali huyo anajua akifanyacho na pia
 
anajiamini katika kazi yake,Madee amefunguka na kusema hayo alipokuwa akicha Live kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live.
Madee aliongeza kuwa licha ya Ney wa Mitego kumletea upinzani juu ya cheo chake cha Raisi wa Manzese lakini bado ataendelea kuwa Rais wa manzese kwa sababu dunia nzima inatambua kuwa Madee ndiyo Rais wa Manzese na kamwe haitakuja kujirudia maana hakuna uchaguzi mwingine uliofanyika na kamwe hautakuja fanyika hivyo yeye ndiye Rais wa manzese. "Madee Seneda ndio rais wa manzese na dunia yote inalijua ilo,vilevile uchaguzi mwengine haujafanyika na hautafanyika tena,so nitaendelea kuwa raisi wa Manzese"
Mbali na hilo Madee amejaribu kuweka wazi kuwa alikuwa akitofautiana kimashairi na mfalme wa Rhymes Afande Sele katika nyimbo zake mbalimbali na kuonekana kumdissi mkali huyo lakini haikuwa ugomvi wa watu kupigana au kushikana mashati,kama ambavyo watu wengi wamekuwa wakihisi kuwa watakuwa na bifu kubwa kati yao,na kuonesha kuwa walikuwa hawana bifu la namna hiyo Madee amesema amefanya kazi na Afande Selle na muda si mrefu kazi hiyo inaweza kutoka.
"Sikuwa na bifu kihivyo na Afande Selle bali tulipishana kimashairi tu na sio ugomvi wa ngumi au kushikana mashati ,namueshimu sana Baba Tunda na pia naeshimu muziki wake,hivyo watanzania kaeni tayari kwa ngoma ya Madee na Afande selle siku za karibuni"
SITUKANI KWENYE NYIMBO
Rais wa Manzese ambaye Video yake ya Tema mate tuwachape ilipigwa marufuku kuoneshwa katika Televisheni na Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) kutokana na video hiyo kukiuka tamaduni na maadili ya Kitanzania,amesema kuwa katika nyimbo zake yeye hatukani matusi ndiyo maana nyimbo hizo zinaendelea kuchezwa katika vituo mbalimbali vya Radio nchini na nje ya Tanzania.

HIP HOP HAIKUNIPA MAFANIKIO
Madee ambaye awali alikuwa akifanya muziki aina ya Hip Hop na baadae kuichana iana hiyo ya muziki kwa kuiandikia ngoma iliyokwenda kwa jina la Hip Hop haiuzi amedai kuwa alifanya Hip Hop lakini hakuna alichokipata katika muziki huo ndio maana ameamua kuachana nao na kufanya muziki unapendwa na watu ambao umeweza kumpa mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi,ukilinganisha na muziki wa Hip Hop alioufanya kwa muda mrefu bila mafaniko yoyote.

NGOMA MPYA
Madee amesema kuwa kwa sasa yupo teyari kuachia ngoma nyingine mpya baada ya ngoma yake ya Tema mate kufanya poa kwa muda mrefu,hivyo anatarajia kuachia wimbo mpya mwishoni wa mwezi huu Tarehe 27,mbali na hilo mkali huyo ameweka wazi kuwa anatamani sana kufanya kazi na msanii anayeiwakilisha Ilala katika game Chid Benz.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE