June 01, 2014

Mzee Stephen Wassira akimpa Zitto pole na faraja katika msikiti wa Maamur.Picha kwa hisani ya Khalfan Said. 

 Mzee Stephen Wassira akimpa Zitto pole na faraja katika msikiti wa Maamur.Picha kwa hisani ya Khalfan Said.

Maiti ya Bi Shida Salum, mama mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, imesafirishwa kwenda nyumbani Kigoma kwa ajili ya mazishi.


Maiti aliombewa dua kwenye msikiti wa Maamur ulioko Upanga jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwa ndege kwenda kwao Kigoma.
Kwa mujibu wa familia, Bi Shida atazikwa kesho Jumatatuumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, atazikwa Jumatatu (Juni 2) huko Mwanga-Kisangani baada ya salama ya mchana.
Shida alifariki mapema saa tano asubuhi (Jumapili, Juni 1), akiwa na umri wa miaka 64, katika hospitali ya AMI, iliyoko Masaki jijini Dar es Salaam, alikokuwa akitibiwa kansa ya kizazi.
Awali mama yake Zitto alikuwa amepelekwa kuhojiwa India kabla ya kurejeshwa nyumbani wiki kadhaa zilizopita na kuendelea kutibiwa katika hospitali ya AMI.
Bi Shida ambaye hadi anaaga dunia alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Walemavu nchini, pia alikuwa mjumbe wa bunge maalum la katiba ambalo sasa liko mapumziko.
Vile vile mama yake Zitto alikuwa na wadhifa mkubwa ndani ya CHADEMA, akiwa mjumbe wa Kamati Kuu.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE