Mtoto wa Pele afungwa jela miaka 33 Brazil
Gwiji wa soka Pele akionekana mwenye huzuni.
Kijana huyo wa gwiji Pele alikuwa akiichezea klabu ya zamani ya baba yake ya Santos katika miaka ya 1990.
Edinho, ambaye kwa sasa anafanya kazi kama mwalimu wa walinda milango (makipa) Santos, iliripotiwa akisema kuwa yeye ni mwathirika wa dawa za kulevya na kukataa mashtaka ya kuwa anasafirisha.
Vyombo vya habari vya Brazil havikuweza kumpata Edinho, ambaye jina lake halisi ni Edson Cholbi do Nascimento. Anatarajiwa kukata rufaa.
Mchawi soka (kama watu wanavyopenda kumuita) Pele akiwa na familia yake.
Alikuwa mlinda mlango wa Santos mwaka 1995 wakati timu hiyo ilipofikia fainali ya ligi ya Brazil na kupoteza taji kwa Botafogo.
Mwaka 2006, Pele alimtembelea kijana wake gerezani na kusema; “Mungu akipenda, haki itapatikana. Hakuna ushahidi wowote dhidi ya mwanangu.
Pele alishinda Kombe la Dunia la mwaka 1958, 1962 na 1970 na alitajwa kama mchezaji nguli kwenye kizazi chake
Source:taarifa.co.tz
0 MAONI YAKO:
Post a Comment