July 11, 2014

Virusi vya HIV
Mtoto mmoja nchini Marekani ambaye alidhaniwa kuwa mtu wa kwanza nchini humo kutibiwa virusi vya HIV akiwa mtoto, amepatikana tena kuwa na virusi hivyo.
Mtoto huyo mwenye umri wa miaka minne kutoka jimbo la Mississipi amekuwa bila ya virusi hivyo kwa zaidi ya miaka miwili baada ya kupata matibabu maalum akiwa bado mtoto mdogo.
Kisa chake kiliibua matumaini makubwa ya tiba ya ugonjwa wa ukimwi.
Madaktari wanasema kuwa kuibuka tena kwa virusi hivyo kumewasikitisha sana.
Madaktari walimpima mtoto huyo na kugundua kuwa angali ameambukizwa virusi vya HIV.
Mwezi Machi mtoto huyo alipopimwa hakupatikana na virusi ikizingatiwa kuwa hakuwa anapokea matibabu kwa karibu miaka miwili.
Bila shaka taarifa hii ni pigo kwa matumaini ya matibabu kutoweza kumaliza virusi vya HIV mwilini kabisa.

Related Posts:

  • MVUA ZALITESA JIJI LA DAR Mburahati na Mayfair leo asubuhi Tokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbali mbali ya Dar es Salaam, zimepelekea uharibufu wa barabara na mazingira. Haya ni maeneo ya jiji la Dar es Salaam yaliyoathirika … Read More
  • JUMA NATURE ASEMA JOKATE MWEGELO AMEMUIGA Chelewa chelewa, utakuta mwana sio wako!! Ndicho kilichotokea kwa Juma Nature ambaye wazo lake la kuanzisha ndala liliendelea kuwa la mdomoni na ‘kutalk the talk’ ilhali Jokate Mwegelo akileta action kweli kwa ‘kuwalk t… Read More
  • MVUA MOROGORO ZAIDI YA MASAA 24, ZALETA ATHALI KWA WANANCHI Wananachi wa kata ya Mwembesongo wakitemebe kwenye maji baada ya barabara ya kichangani kujaa maji wakitoa maji yaliyojaa dukani kwao  Bi,Hasma Ndehele ambaye ni Kigogo wa CCM kata ya Mji Mpya ak… Read More
  • TB JOSHUA: UTABIRI WAKE WATIMIA Prophet TB Joshua alitabiri mwaka jana kwamba Nigeria itakua ya kwanza kiuchumi kushinda nchi zote za Africa. Wakati anatabiri. ..nilikua nikiangalia nchi ya Africa Kusini, Misri etc.....niliwaza sana. Jana Imetangazwa kuw… Read More
  • PATA MUDA WA KUANGALIA VIDEO MPYA YA QUEEN DARLEEN NA SHILOLE   Hii ni video iliyowahusisha Diamond Platnumz na dada yake wa damu  Queen Darlin uzinduzi wa video hii ulifanyika Bilicanas mwishoni mwa wiki iliyopita,video hii imetenegezwa na kampuni ya Jerry Mushala Stud… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE