AZAM FC: HATUJAINGIA MKATABA NA CHUJI, AMEOMBA KUFANYA MAZOEZI Kitaifa
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
BAADA ya taarifa kuenea mchana wa
leo kuwa aliyekuwa kiungo mzoefu wa Yanga, Athumani `Idd Chuji`
amesajiliwa na Azam kutokana na kuonekana katika mazoezi ya klabu hiyo
kwenye uwanja wa Azam Complex, uongozi wa mabingwa hao umekanusha
taarifa hizo.
Chuji aliyetemwa na Yanga
alionekana katika jezi ya Azam fc, lakini msemaji wa klabu hiyo, Jafar
Idd Maganga amesema klabu hiyo haijaingia mkataba wowote na kiungo
huyo.
Jafar aliongeza kuwa Chuji
aliomba kufanya mazoezi na Azam na kwasababu klabu hiyo inapenda michezo
haikuona sababu ya kumnyima nafasi hiyo.
“Chuji aliomba kufanya mazoezi, uongozi ukaona si jambo la busara kumkatalia”. Alisema Jafar.
“Hata katika mazoezi ya leo jezi aliyovaa haikuwa na namba yoyote, kwahiyo hatuna mkataba wowote”.
Jafar alisisitiza kuwa jioni ya
leo ameongea na katibu mkuu wa klabu hiyo, Nassor Idrissa `Father` na
alielezwa kuwa hakuna mkataba wowote ambao Azam fc imeingia na Chuji
zaidi ya kuomba kufanya mazoezi.
‘Kuvaa jezi ya Azam sio kwamba
ndio tumemsajili, sisi tunaenda kisasa. Tunapofanya mazoezi, timu moja
inavaa jezi na timu nyingine inavaa jezi. Kama mchezaji yupo mazoezini
lazima avae jezi, lakini hatuna mkataba na mchezaji huyo”.
Hata hivyo, Jafar alisema suala
la Chuji kusajiliwa itategemeana na mwalimu atamuonaje katika mazoezi na
kama ataonekana ana kiwango kizuri, kazi ya uongozi ni kutekeleza
mahitaji ya mwalimu.
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
BAADA ya taarifa kuenea kuwa aliyekuwa kiungo mzoefu wa Yanga, Athumani `Idd Chuji` amesajiliwa na Azam kutokana na kuonekana katika mazoezi ya klabu hiyo kwenye uwanja wa Azam Complex, uongozi wa mabingwa hao umekanusha taarifa hizo. Chuji aliyetemwa na Yanga alionekana katika jezi ya Azam fc, lakini msemaji wa klabu hiyo, Jafar Idd Maganga amesema klabu hiyo haijaingia mkataba wowote na kiungo huyo. Jafar aliongeza kuwa Chuji aliomba kufanya mazoezi na Azam na kwasababu klabu hiyo inapenda michezo haikuona sababu ya kumnyima nafasi hiyo. “Chuji aliomba kufanya mazoezi, uongozi ukaona si jambo la busara kumkatalia”. Alisema Jafar. “Hata katika mazoezi ya leo jezi aliyovaa haikuwa na namba yoyote, kwahiyo hatuna mkataba wowote”. Jafar alisisitiza kuwa jioni ya leo ameongea na katibu mkuu wa klabu hiyo, Nassor Idrissa `Father` na alielezwa kuwa hakuna mkataba wowote ambao Azam fc imeingia na Chuji zaidi ya kuomba kufanya mazoezi. ‘Kuvaa jezi ya Azam sio kwamba ndio tumemsajili, sisi tunaenda kisasa. Tunapofanya mazoezi, timu moja inavaa jezi na timu nyingine inavaa jezi. Kama mchezaji yupo mazoezini lazima avae jezi, lakini hatuna mkataba na mchezaji huyo”. Hata hivyo, Jafar alisema suala la Chuji kusajiliwa itategemeana na mwalimu atamuonaje katika mazoezi na kama ataonekana ana kiwango kizuri, kazi ya uongozi ni kutekeleza mahitaji ya mwalimu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment