July 10, 2014


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhipZuIZZtbE7QUb0B4AJyLwwP9dYlHbAh2VB68MKLdQi83yjzEW2SGxeeodzgvL_DiLFq3LWzYzpm2lDHRemuRNB-DEoIW4JBXwgifblACJZY8YQMIjXlAEtdWI2Wwapec0a_5n7eM_rVd/s1600/1.jpg
STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amefanya tukio la kihistoria
kiasi cha kumliza mama yake mzazi, Sanura Kassim ambaye alimwaga machozi kama mtoto mbele za watu.
KILICHOMLIZA Muda mfupi baada ya shughuli ya kufuturu kukamilika, mama Diamond alishangaa kusikia kwamba kulikuwa na jambo jingine la ziada katika siku hiyo. Alitolewa nje huku akiimbiwa ‘happy birthday’ ndipo alipogundua kilichokuwa kikiendelea.Mara baada ya shampeni isiyo na kilevi kufunguliwa na waalikwa kupewa, meneja wa Diamond, Babu Tale na wapambe wengine walimuongoza mama huyo hadi kwenye gari aina ya Toyota Lexus Harrier na kuelezwa kuwa ni mali yake kuanzia muda huo tamko lililomshtua na kuanza kulia akiwa haamini alichosikia!
WEMA, AUNT WAMBEMBELEZA Wema Sepetu na staa wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel walipovaa jukumu la kumtuliza.
DIAMOND, WEMA NDOA LAZIMA! Katika kuonesha kuwa sasa amekubali kwa dhati Wema awe mkwewe, mama Diamond aliapa lazima ahakikishe mwanaye anafunga ndoa na mlimbwende huyo.
“Hilo nataka mlijue kabisa. Nitafanya juu chini Diamond amuoe Wema maana ana roho nzuri sana. Niseme ukweli kuwa huyu msichana ndiye chaguo langu na wanaendana sana na mwanangu. “Angalia wakiwa pamoja, mwanangu anapata mafanikio makubwa sana, nadhani nyota zao zinaendana hivyo sina pingamizi lolote. Ninachotaka ni kuhakikisha wanaoana,” alisema mama Diamo

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE