July 19, 2014

  Fabio Borini, 23, anajiandaa kujiunga na Sunderland baada ya Liverpool kukubali ada ya pauni milioni 14 (Sky Sports), baada ya kumchukua Filipe Luis siku ya Ijumaa, Chelsea wanazungumza na Atlètico Madrid kuhusu kumsajili beki kutoka Brazil Joao Miranda, 29 kwa pauni milioni 20 (Daily Star), Real Madrid wanafikiria kumchukua Alvaro Negredo, 28, kutoka Manchester City kuziba nafasi ya Alvaro Morata, 20, anayekwenda Juventus (Metro), Liverpool wamemwambia Loic Remy, 27 kupunguza madai ya mshahara mkubwa kama anataka kufanikisha uhamisho wake wa pauni milioni 8 kutoka QPR (Daily Mirror), QPR wamepewa nafasi ya kumsajili Samuel Eto'o lakini huenda wakakataa kutokana na kutokubaliana mshahara (Daily Mail), Arsenal watakabiliwa na ushindani kutoka Valencia kumsajili kipa David Ospina, 25 (Metro), Everton wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili Romelu Lukaku, 21, kutoka Chelsea kwa uhamisho wa kudumu (Daily Mail), Tottenham wanakaribia kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 10 wa beki Ben Davies, 21, kutoka Swansea. Liverpool pia walikuwa wakimtaka (Daily Telegraph), boss wa QPR, Harry Redknapp amesema anapanga kusajili wachezaji "sita au saba" zaidi kabla ya kuanza msimu mpya (Times), AC Milan wapo tayari kusubiri mwisho wa dirisha la usajili kuanza kumfuatilia Nani ambaye Manchester United wanataka euro milioni 14 (Corriere dello Sport).

Related Posts:

  • Wanawake waombwa msamaha wanawake wakifanya maandamano kuadhimisha siku ya wanawake duniani nchini Indonesia   Kampuni inayotengeneza nguo za riadha nchini Indonesia, imeomba msamaha, kwa kuuza t-shat… Read More
  • Ubunge Morogoro Mjini, hatimaye Maharagande avaa gwanda rasmi   Maharagande akipokea fomu za kuwania nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea wa ubunge morogoro mjini kutoka kwa katibu kata ya Sultani Area Amin Kabwanga katikati, wanaoshuhudia tukio hilo kushoto ni M/kiti CUF  Moro… Read More
  • Rais Kikwete ajivunia kuwabeba wanawakeRais Jakaya Mrisho Kikwete amesema anajivunia kuona anamaliza muda wake akiwa amefanikisha kujenga msingi imara ya kuwawezesha na kuwapa nafasi wanawake katika ngazi za uongozi na hivyo kuwataka viongozi wajao waendelee kuwap… Read More
  • Chinja chinja wa IS alikuwa mlevi   Mohammed Emwazi ,mtu ambaye alibadilika na kuwa ''chinja chinja'' wa kundi la islamic state kwa jina 'jihad John' Mohammed Emwazi, alifurushwa kutoka nchini Tanzania kwa kuwa mlevi na mtu anayetoa matusi.,afisa m… Read More
  • Mtatiro: Nitagombea Ubunge Segerea   Ndugu zangu, kesho Jumatatu 09 Machi 2015 saa 4.00 asubuhi, nitachukua fomu ya kuwania ubunge katika jimbo la Segerea kama ambavyo taratibu za ndani ya chama changu zinaruhusu. Hakutakuwa na mbwembwe vifijo wala … Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE