
Yanawezekana
yakawa ni moja ya mauaji ya kutisha nchini, baada ya kijana mmoja
kumuua mwanafunzi wa darasa la tatu Shule ya Msingi ya Marangu Hills
Academy kisha kula ubongo wake.
Mbali
na kula ubongo wa mtoto huyo, Francis Urassa (9), mtuhumiwa huyo
Lawrence Mramba alijikata sehemu za siri kwa kutumia wembe na kuzila
mithili ya mshikaki akikata kipande kimoja baada ya kingine.
Hata
hivyo, mtuhumiwa huyo naye alifariki dunia saa chache baadaye baada ya
kufikishwa Hospitali ya Kilema iliyopo Moshi Vijijini wakati madaktari
na wauguzi wakimpatia matibabu.
Mashuhuda
wa tukio hilo lililotokea jana saa 1:00 asubuhi Kijiji cha Samanga,
Wilaya ya Moshi Vijijini, walidai kijana huyo alikuwa na nguvu za ajabu
lakini baadae polisi walifanikiwa kumdhibiti.
Wananchi
walipiga simu polisi kuomba msaada baada ya kijana huyo aliyekuwa na
panga kuwazidi nguvu na kubakia watazamaji wakimwangalia namna
anavyokula nyama za mwili wake.
Lilikuwa
ni tukio lililovuta hisia za wakazi wengi waliokusanyika kijijini hapo
huku wengine wakirekodi tukio la kijana huyo kula uume wake kwa kutumia
simu za mikononi.
Polisi
kutoka Mji wa Himo walifika eneo la tukio na kumkamata kijana huyo
wakati huo akiwa katika hali mbaya kutokana na kupigwa kwa mawe na
wananchi na kujikata sehemu mbalimbali.
Mwili
wa kijana huyo ulionekana ukiwa umetapakaa damu kuanzia mdomoni hadi
sehemu za siri kutokana na damu nyingi kuchuruzika wakati akijikata uume
vipande vipande na kuula.
RPC Kilimanjaro anena
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz aliliambia gazeti hili jana
kuwa chanzo cha tukio hilo ni upungufu wa akili uliomkumba kijana huyo
na kuanza kuvunja vioo vya nyumba.
“Leo
(jana) asubuhi alimkata huyo mtoto wa tajiri yake kwa panga na kisha na
yeye akaanza kujikata sehemu zake za siri na kula baadaye akajikata pia
sehemu mbalimbali za mwili,” alisema.
Kwa
mujibu wa Kamanda Boaz, mtuhumiwa huyo alifariki katika Hospitali ya
Kilema iliyopo Wilaya ya Moshi Vijijini wakati madaktari na wauguzi wa
hospitali hiyo wakimpatia matibabu
Mtendaji wa kijiji asimulia
Ofisa
Mtendaji wa Kijiji cha Samanga, Vick Lyimo alisema siku moja kabla ya
mauji hayo, kijana huyo aliyekuwa akijifunza kazi ya Useremala
alionekana kuchanganyikiwa kiakili.
Kutokana
na kuchanganyikiwa huko, tajiri yake aitwaye Fortunatus Urassa ambaye
ni baba wa marehemu, alimchukua na kumpeleka nyumbani kwake kwa ajili ya
kupumzika.
Hata
hivyo, mtendaji huyo alidai jana saa 1:00 asubuhi, wakati mtoto wa
tajiri yake akitoka nyumbani kwenda shule alimvamia na kumpasua kichwa
kwa panga na kisha kula ubongo wake.
“Sasa
baada ya kula huo ubongo ndio akaanza kujitaka uume wake kipande kwa
kipande na kukila mpaka polisi walipofika kwa vile alikuwa akitishia
watu kwa panga,” alisema mtendaji huyo.
Mchungaji wake ashikwa na butwaa
Mchungaji
Ebeneza Ngomuo wa Kanisa la Pentecoste Marangu alikokuwa akisali
mtuhumiwa alisema haamini kilichotokea kwa vile muumini wake huyo
alikuwa ni mtu mpole na mtaratibu.
“Ni
tukio la kusikitisha na siamini kama huyu kijana yuko sawasawa kwa vile
kabla ya tukio alikuwa anaonekana mara zote ni mpole, mtaratibu na
asiyetumia kilevi,” alisema mchungaji huyo.
“Sisi
kama kanisa tumepata mshangao lakini naamini huu ni mpango wa shetani
kwa hali ya kawaida kijana huyo hawezi kufanya unyama huu,” aliongeza
mchungaji huyo na kusema;
“Siyo
jambo rahisi mtu kula nyama ya binadamu mwenzie na yeye mwenyewe kula
nyama zake zikiwamo sehemu za siri... lilikuwa ni tukio baya sana
kuliona.”
Mtoto aliyeuawa alikuwa na uwezo kwenye masomo
Mwalimu
wa Shule ya Marangu Hills Academy alikokuwa akisoma mtoto Francis,
Thomas Malulu alisema tukio hilo ni la uchungu na limewaumiza sana wao
kama familia ya shule hiyo.
“Tukio
hili ni la uchungu sana kwetu na familia ya Francis. Alikuwa ni mtoto
mwenye kipaji darasani na kwa kweli tukio hili limezima ndoto
yake,”alisema mwalimu huyo.
Mwalimu
huyo alisema tukio hilo limeacha kumbukumbu ambayo itawachukua muda
mrefu kuwatoka na kusisitiza kuwa wao kama wanadamu hawana la kufanya
zaidi ya kumwachia Mungu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment