Kwa
mujibu wa mtu wa karibu wa Jack, modo huyo alihukumiwa Jumatatu
iliyopita (Agosti 11, mwaka huu) kwenye Mahakama ya Macau huko Hong Kong
ambapo hukumu hiyo ilitofautiana na adhabu nyingine za madawa nchini
humo ambazo huwa hukumu yake ni kunyongwa hivyo ya Jack kuonekana
nyepesiii!
Kikizungumza
na Globalpublishers chanzo hicho makini kilidai kwamba, hukumu hiyo ya
Jack ni nyepesi ukilinganisha na hukumu nyingine za madawa ya kulevya
zinazotolewa nchini China ambapo hakimu alitumia muda wa dakika 27 tu
kuisoma.
“Hukumu
za madawa ya kulevya zinatofautiana nchini China. Kuna baadhi ya
majimbo kama Beijing huwa wao ikithibitika umebeba madawa ya kulevya,
unanyongwa lakini baadhi ya maeneo unafungwa miaka kadhaa. Miaka
hutofautiana kulingana na sheria walizojiwekea,” kilifunguka chanzo chetu.
Ilidaiwa
kwamba, kwa mujibu wa hukumu hiyo aliyohukumiwa mrembo huyo, anaweza
kupunguziwa muda wa kifungo kulingana na nidhamu atakayoionesha gerezani
kama mahakama ilivyoelekeza.
“Anaweza
akapunguziwa kifungo kwa sababu hukumu imeeleza wazi kwamba anaweza
kupunguziwa adhabu hiyo kama atatimiza masharti ya kinidhamu ambayo
sheria za China zinamtaka atimize,” kilisema chanzo hicho.
TUJIUNGE NA CHANZO
“Amehukumiwa juzi Jumatatu, ametakiwa kwenda jela miaka sita,
nilikuwa nikiwasiliana naye mara kwa mara lakini juzi hiyo ndiyo
kanitumia taarifa kwamba amehukumiwa na kunieleza kwamba siku hiyo
aliduwaa kwa muda maana hakuamini kama anaweza kuhukumiwa kwani alikaa
muda mrefu bila kujua hatima yake,” kilisema chanzo hicho kilicho karibu na Jack.
JACK AFURAHIA HUKUMU
Chanzo
hicho kilizidi kumwaga data kuwa, baada ya hukumu hiyo kupitishwa, Jack
alifurahia hususan kuwepo kwa kipengele cha uwezekano wa kupunguziwa
kifungo kama atakidhi masharti aliyopewa na mahakama.
“Baada
ya kutafakari kwa kina hukumu yake, Jack anaonekana kuifurahia kwa
sababu anaamini kwake yeye itakuwa ni rahisi kutimiza masharti ya kuwa
mstaarabu kadiri kipengele hicho kilivyomuelekeza,” kilisema chanzo.
NDUGU HAWAJUI LOLOTE?
Katika
hatua nyingine, chanzo hicho kilifunguka kuwa ndugu wa Jack waliopo
Tanzania hawakuwa na taarifa zozote kuhusiana na hukumu hiyo.
Kilisema
kuwa kwa upande wake iliwezekana kupata haraka taarifa hizo kwani
alikuwa akiwasiliana na Jack mara kwa mara kwa njia ya barua. “Ilikuwa
ni rahisi mimi kunipa taarifa hizi haraka kwa sababu nilikuwa
nikiwasiliana naye mara kwa mara, labda sasa hivi kwa kuwa nawapa ninyi
(waandishi wetu) hizi taarifa ndiyo wanaweza na wao kujua
kinachoendelea,” kilisema chanzo hicho.
NDUGU WASAKWA
Jitihada
za kuwatafuta ndugu wa Jack waishio jijini Dar hazikuzaa matunda kwani
namba zao za simu zilikuwa hazipatikani. Hata hivyo, rafiki wa karibu
wa familia ya Jack ambaye hakutaka jina liandikwe alisema wamezipokea
habari hizo kwa furaha kwani kulikuwa na hofu kubwa kuwa huenda ndugu
yao akanyongwa.
“Ndugu,
jamaa na marafiki wa karibu na Jack wameipokea hukumu hiyo kwa furaha
maana walikuwa wakihofia adhabu ya kunyongwa ambayo inatolewa zaidi
nchini China,” alisema rafiki huyo wa familia.
TUJIKUMBUSHE
Jackie
alikamatwa Desemba 19, mwaka jana akiwa amebeba madawa ya kulevya aina
ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau
akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa
Jimbo la Guangdong Kusini mwa China.
source: Globalpublishers
0 MAONI YAKO:
Post a Comment