August 05, 2014

Kanda inayoonyesha msimamizi mkuu wa makao ya kuwatunza watoto mayatima nchini Misri akiwachapa watoto hao walio chini ya ulinzi wake, imezua hasira miongoni mwa watu wengi nchini humo.
Rais Abdel Fattah Al-Sisi aliingilia kati kashfa hiyo na sasa msimamizi huyo amekamatwa.
Kanda iliyofichuliwa ilionyesha, watoto hao walio kati ya umri wa miaka minne na saba wakiangua kilio huku meneja huyo akiwachapa kwa mwiko.
Mkewe meneja huyo aliambia kituo cha televisheni cha Misri kuwa alirekodi kanda hiyo mwaka mmoja uliopita kwani hangeweza tena kukaa kimya wakati ukatili huo ukiendelea.
''Yeye huchapa kila mtu ikiwemo wanangu na hata mimi mwenyewe, '' alisema mama huyo.
Katika kanda hiyo, mwanamume huyo anaonekana kuwaadhibu watoto hao kwa sababu eti waliwasha televisheni na kufungua jokofu bila ya idhini yake.
'Bila huruma'
Kanda hiyo ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii Jumapili. Kwa siku moja tu kanda hiyo ilikuwa imetazamwa na zaidi ya watu 20,000 kwenye YouTube na kupitia Facebook iliweza kutumwa kwa watu wengine angalau mara 85,000.
Watoto hao mayatima sasa wamehamishwa hadi katika makao mengine, aliyowahamisha akisema watoto hao wako huru sasa utadhani wamondoka gerezani.
Gavana wa mkoa wa Giza pia amefunga rasmi makao hayo kwa mujibu wa shirika la habari la Nile News TV.
Baadhi ya vyombo vya habari vimetoa wito wa meneja huyo kuadhibiwa.
"kupitia kwa video na picha:meneja wa makao ya kuwalinda watoto, ameoenekana akiwaadhibu watoto wadogo kwa kutizama TV , hilo halifai,'' alisema mkuu wa shirika la habari la Al-Watan. ''
Visa vya dhuluma dhidi ya watoto wanaoishi katika makao ya kuwatunza watoto, vimesemwa sana ingawa havijaipotiwa kwenye vyombo vya habari nchini Misri.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE