pikipiki yake haikuumia sana kama inavyonekana pichani
Askari usalama barabarani akisimamisha magari yanayotokea upande wa Dodoma kupisha wenzake kupima eneo hilo la tukio
wakipima eneo hilo la tukio
Mwili wa marehemu na pikipiki yake kwa pamoja vilipakiwa kwenye Gari ya Polisi
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
WIMBI la vifo vitokanavyo na usafiri
wa pikipiki maarufu 'Bodaboda' kuziki kushika kasi kote nchini wananchi
mkoani hapa wanaendelea kuhoji bodaboda hizo zimekuja nchini
kuwasafirisha au kuwasafisha,kauli hiyo imesikika jana eneo la Kihonda
Oil Com baada ya dereva wa boda bodoa kugongwa na basi dogo aina ya
Coaster na kufa papo hapo.
Habari zilizopatikana eneo la tukio
zilidai kwamba boda boda huyo aliyefahamika kwa jina moja la lsaya anaye
egesha pikipiki yake kijiwe cha Oil com njia panda ya Kihonda
Maghorofani kando kando ya barabara kuu ya Morogoro-Dodoma,aligongana na
daladala hiyo inayofanya safari zake Kihonda- Mjini na kufa papo hapo.
Shuhuda wa tukio hilo
aliyejitambulisha kwa jina la Jumanne Kudula alisema" lssaya alitoka
hapa kijiweni na kuingia barabara kuu ya Moro-Dodoma akiwa peke yake na
kwamba mbele yake kulikuwa na msafara wa magari zaidi ya saba yaliokuwa
yakienda kuzika, alijaribu kuyapita kwa magari hayo kwa bahati
mbaya alikutana uso kwa uso na Coastar aliyogongana nayo uso kwa uso
lsaya alipasuka kichwa na ugongo kumwagika kwenye Lama"alisema shuhuda
huyo kwa uchungu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment