Robin William ni star aliyeanza kupata mafanikio akifanya kazi kama stand up comedian na baadae kuanza kuonekana kwenye movie.
Akiwa na miaka 63 Robin amefariki dunia kwa kifo ambacho hadi
sasa hakijajulikana chanzo chake lakini tetesi zinasema kuna uwezekanao
kwamba Robin alijiua.
Mwili wake umekutwa nyumbani kwake huko Tiburon California na
watu wa karibu wanasema alikuwa anasumbuliwa na msongo wa mawazo hivi
karibuni.
Enzi za uhai wake aliwai kushiriki kwenye movie kama The Fisher King,Good will Hunting,Jumanji,Popeye na nyingine.
Pia alishinda tuzo kama Academy,Golden Globe,Emmy,Grammy na nyinginezo kwa wakati tofauti.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment