Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera ACP Henry Mwaibambe
Watoto
wawili wa kijiji cha Rwerere kata Rwambaizi wilayani Karagwe Noviath
Sarapion(14) na Kalen Dausoni ( 4) wamefariki dunia baada ya kunywa sumu
ya kuoshea mifugo, wakidhani ni dawa ya kutibu kikoozi.
Tukio hilo limetokea majira ya saa Nne asubuhi August 10 mwaka
huu(Jumapili) katika kijiji hicho, huku mama yao akiwa ameenda kanisani
kusali, na baba yao Sarapioni Gondo akiwa ameenda kusalimia majirani.
Mama yao aliyejulikana kwa jina la Mama Subi (35) ameeleza kuwa
watoto hao ambao ni marehemu kwa sasa walikuwa wanasumbuliwa na kikoozi
ambapo walichanganya chupa ya dawa ya mifugo badala ya dawa kikoozi
iliyokuwa chumbani na kuinywa,wakiwa na dhumuni ya kutibu kikoozi
walichokuwa nacho.
Katika harakati zakuokoa maisha ya watoto hao, mtoto mdogo Kaleni
alifia katika Kituo cha afya cha Rwambazi kabla ya kupatiwa huduma,
ambapo Noviathi aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la Saba shule ya msingi
Rwele alifia njiani akikimbizwa katika hopitali ya wilaya Nyakahanga.
Kutokana na kuwepo tukio hilo la kuhuzunisha, jeshi la Polisi mkoani
hapa,limewatahadharisha wananchi wote kuepuka kuchanganya dawa za
matumizi tofauti katika makazi yao, huku likisisitiza umuhimu wa kuweka
wazi matumizi ya dawa hizo kwa wanafamilia.
Kamanda wa jeshi hilo mkoani hapa Henry Mwaibambe, akitoa maelezo
juu ya vifo hivyo, amewataka wananchi kuondoa dhana ya usiri na
kuelimisha jamii kwa kila jambo ili kuweza kuepuka madhara yanayoweza
kutokea.
Wazazi wanapaswa kujitahidi kuendelea kuwaelimisha watoto kama kuna
dawa imenunuliwa kwa malengo fulani kabla ya matumizi jitahidi kutoa
maelezo kwa watoto na pia dawa ziwekwe mbali na watoto kama maelezo ya
dawa yanavyoelezwa na dawa yoyote inaweza kuwa sumu ikiwa imetumika
visivyo alisema Mwahibambe.
Kwa mujibu wa Kamanda Mwaibambe, tayari miili ya marehemu imekabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment