Wastara Juma
Mwigizaji maarufu wa filamu hapa Bongo, Wastara Juma ameweka wazi kuwa baada ya kukamilika kwa filamu yake mpya ya Last Decision, amejipanga kwaajili ya uzinduzi wa aina yake ambao ataufanya mitaani pamoja na mashabiki wake ndani ya siku 5 zijazo.
Wastara
amesema kuwa, atatumia siku nzima katika kuzindua kazi hii katika
wilaya za jiji la Dar pamoja na kukutana na mashabiki wake ambao kwa
asilimia kubwa wanapatikana huko mitaani.
Wastara pia katika mahojiano tuliyofanya naye, amekanusha taarifa za
yeye kupata mchumba na kuolewa huko Uingereza, na kufafanua kuwa picha
zilizokuwa zimesambaa mitaani juu ya hili, ni kutoka katika scene ya
filamu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment