September 18, 2014

Timu ya taifa ya Wales, imeandika historia mpya baada shirikisho la soka duniani FIFA, kutoa orodha ya viwnago vya ubora wa soka vya mwezi huu kwa kuzingatia vigezo vya michezo ya kimataifa iliyochezwa siku za hivi karibuni.
Wales wameandiaha historia hiyo baada ya miaka 20 kupita ambapo wameonekana kukwea kwa nafasi 12 na kufanikiwa kuwakamata ndugu zao Sotland katika nafasi ya 29.
Mafanikio ya kupanda katika viwango hivyo vya ubora duniani yametokana na ushindi wa mabao 2-1 ulioshuhudia Wales wakiinyanyasa Andorra katika harakati za kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2016.
Kwa upande wa timu ya taifa ya Ireland ya Kaskazini imechupa kwa nafasi 24 na kukamata nafasi ya 71 ikiwa ni nafasi tisa nyuma ya Jamuhuri ya Ireland.
Timu ya taifa ya Uingereza imepanda kwa nafasi mbili ikitoka katika nafasi ya 20 hadi katika nafasi ya 18.
Jamuhuri ya Ireland imepanda katika viwango vya ubora kufuatia ushindi wao wa kwanza wa mabao 2-1 wakati wa kampeni za kusaka tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya dhidi Hungary, ili hali timu ya taifa ya Uingereza iliichabanga Uswiz mabao 2-0.
Mabingwa wa soka duniani timu ya taifa ya Ujerumani, imeendelea kusalia katika nafasi ya kwanza, kufuatia ushindi wa mabao mawili kwa moja walioupata dhidi ya Scotland walipoanza kampeni ya kuelekea nchini Ufaransa mwaka 2016.
Hata hivyo kabla ya mchezo huo, Ujerumani waliambulia kisago cha mabao manne kwa mawili mwanzoni mwa mwezi huu, kutoka kwa Argentina lakini haikuharibu mpango wa kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa viwango vya ubora wa soka duniani.
Timu ya taifa ya Colombia nayo imepanda kwa nafasi tatu, ikiziacha timu za taifa za Uholanzi, Ubelgiji, Brazil, Uruguay, Hispania, Ufaransa pamoja na Uswiz zinazotengeneza orodha ya kumi bora.
Orodha kamili ya viwango vya ubora wa soka duniani ambavyo vimetolewa hii leo na shirikisho la soka duniani FIFA Bofya Hapa

Related Posts:

  • Happy Birth day to u Zinedine Zidane   Zinedine Zidane a.k.a Zizou amezaliwa June 23 mwaka 1972 na hadi leo amefikisha miaka 43. Zidane ameoa mwaka 1994 mke wake anaitwa Veronique Zidane. Hadi leo wana watoto wanne ambao ni Enzo Fernandez, Theo Zidane,… Read More
  • Tunda /Tufunge na kuswali -Qaswida   Ikiwa tupo ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, dini ya kiislam wapo kwenye ibada ya Funga, mwanamuziki kutoka Tip Top Tunda mana ameachia Qaswida ikiwa ni sehemu ya kuwaasa waislam kumrejea ,ungu hasa kipindi hik… Read More
  • Mzee Yusuph afichua siri ya mchezo Mfalme wa Taarab nchini na kiongozi wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuph, amesema sababu za bendi yake kupendwa ni utunzi mzuri wa nyimbo zao. Mzee Yusuph ambaye June 13 kwenye tuzo za muziki za Kilima… Read More
  • Ainea kuja na Juddy wiki hii     Mwanamuziki wa kizazi kipya toka mkoani Dodoma Aine wa sinampango naye, yupo mbioni kuachia ngoma yake mpya ya Juddy aliyomshirikisha Dullayo. Akitia Story na blog hii, Ainea amesema ameamua kuja na Dullayo k… Read More
  • AY: awashauri Diamond na Alikiba Rapper Ambwene Yesayah maarufu kama AY ametoa ushauri kwa Diamond na Alikiba kuweka tofauti zao pembeni na kufanya muziki pamoja. AY ametoa ushauri huo baada ya kuulizwa na shabiki kupitia Kikaangoni cha EATV aliyetaka… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE