Mkurugenzi  wa Didas Fashion, Khadija Ayoub Seif, (Wa pili toka Kushoto)  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelezea  uzinduzi wa Filamu ya Mateso Ughaibuni inayotarajiwa kuzinduliwa siku ya  Alhamis Septemba 4, 2014 katika viwanja vya Leadrs Club. Pembeni yake  ni Rais Wa Bongo Movie Steve Nyerere na wasanii wengine.
Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
   FILAMU ya ‘Mateso Ughaibuni’ ambayo  imerekodiwa Uingereza  na wasanii  Issa Musa ‘Cloud 112’,  Riyama Ally,  Wastara Juma  na Monalisa itazinduliwa Alhamisi hii katika viwanja vya  Leaders, jijini Dar es Salaam.Akizungumza  na waandishi wa habari jijini  Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Didas Fashion, Khadija Ayoub Seif,  ambaye  kampuni yake ndiyo iliwapeleka wasanii hao Uingereza kwenda kurekodi  filamu hiyo, alisema licha ya  kampuni yake kujihusisha na mambo ya  mavazi na vitu vingine ameona kuna kila sababu ya kuwasaidia Watanzania  wanaofanya  sanaa  ya uigizaji.  
 
Rais  wa Bongo Movie Steve Nyerere akiongea machache mbele ya waandishi wa  habari juu ya uzinduzi wa Filamu ya Mateso Ughaibuni. Pembeni yake ni  Mkurugenzi wa Didas Fashion, Khadija Ayoub Seif na      

 
Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini.
 
 
Wafanyakazi wa PSPF nao walikuwepo kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.
TAZAMA KWA UFUPI HAPA
TAZAMA KWA UFUPI HAPA





0 MAONI YAKO:
Post a Comment