Mkuu
wa Wilaya (DC) Temeke, Mheshimiwa Sophia Mjema akihutubia kwa niaba ya
mke wa waziri mkuu, Tunu Pinda, aliyetarajiwa kuwa mgeni rasmi,
(hakufika) wakati wa uzinduzi wa filamu hiyo.
Muigizaji Esha Buheti akiwa katika zulia jekundu 'red carpet' kwa ajili ya kupiga picha kwenye uzinduzi wa filamu hiyo.
Mkurugenzi
wa Didas Fashion, Khadija Ayoub (mwenye gauni la zambarau) akiwa katika
picha ya pamoja na Mkurugenzi wa The Mboni Show, Mboni Masimba wakati
wa uzinduzi huo.
Muigizaji Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’ akitoa neno la shukrani kwenye uzinduzi huo.
Baadhi ya wasanii wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa filamu hiyo.
Mwanamuziki
wa Bongo Fleva, Feisal ‘Mweupe’ akiwa katika picha ya pamoja na
Mkurugenzi wa Didas Fashion (kulia) ambaye amejitolea kusimamia kazi
zake, katikati ni rafiki yao.
Msanii wa Bongo Muvi anayejulikana kwa jina la Najma akiselebuka na midundo ya Bendi ya Yamoto, nyuma ni Dogo Aslay.
Dogo Aslay akifanya yake wakati wa uzinduzi wa filamu ya Mateso Yangu Ughaibuni.
Wasanii
kutoka Bongo Muvi Idrisa Kupa na mwenzake Chopa wa Mchopanga nao ni
miongoni mwa wasanii waliochizika na Yamoto Band wakati wa uzinduzi
Mmoja wa waigizaji chipukizi katika tasnia ya filamu Bongo, Husna Chobis katika pozi siku ya uzinduzi wa filamu hiyo
H.Baba na Mkewe Flora Mvungi wakiimba kwa pamoja wakati wa uzinduzi wa filamu hiyo.
Rais wa wanenguaji katika muziki wa dansi, Super Nyamwela akiwa na mke wake.
ULE uzinduzi uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na wadau
wakubwa wa tasnia ya filamu Bongo hatimaye umekamilika na kufana ambapo
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, DC Sophia Mjema aliwaongoza wananchi waliofika
kwa wingi kuangalia uzinduzi wa filamu ya Mateso Yangu Ughaibuni
iliyotengenezwa nchini Uingereza chini ya Kampuni ya Didas Fashion.Akizungumza kwa niaba ya mke wa waziri mkuu mama Tunu Pinda, ambaye ndiye alitakiwa kuwa mgeni rasmi, DC Mjema alisema kuwa amefarijika sana kuwepo katika uzinduzi wa filamu ya Mateso Yangu Ughaibuni iliyotengenezwa chini ya Kampuni ya Didas Fashion.
Uzinduzi huo ulifanyika katika Viwanja vya Leaders Club , Kinondoni jijini Dar. “Nimefarijika sana tena ukizingatia pia filamu yenyewe imerekodiwa nchini Uingereza, mimi nadhani hii ni moja ya milango inayofunguka katikia tasnia ya filamu Bongo ambayo inaonekana inatoa ajira kwa vijana kwa wingi” alisema DC Mjema.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment