October 10, 2014

 
Askari polisi watatu wamefukuzwa kazi mkoani Kagera kwa tuhuma za kupiga picha zinazokiuka maadili ya kazi yao na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii jambo linalodaiwa kulidhalilisha jeshi hilo.

  
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe aliwataja waliofukuzwa kazi kuwa ni Mpaji Mwasumbi, Veronica Mdeme na Fadhili Linga.
Kamanda Mwaibambe alisema askari polisi wawili walikuwa Kitengo cha Usalama Barabarani wilayani Missenyi na picha hiyo ilipigwa na askari mwenzao, Fadhili wakati wakiwa kazini mwaka 2012.

Pia, alisema picha iliyoonekana kusambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ni halisi na kudai kuwa watuhumiwa walifanya hivyo wakijua kuwa ni kosa linalokiuka maadili ya kazi yao.

Kamanda huyo alisema mmoja wa askari hao ambaye pia amefukuzwa, aliwapiga wenzake picha hiyo wakiwa kazini kwa kutumia simu yake ya kiganjani na kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE