October 25, 2014

Iran Madam 
Reyhaneh Jabbari mwenye umri wa miaka 26 amehukumiwa kunyongwa baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mtu mmoja ambaye alifanya jaribio la kumbaka.
Taarifa iliyoripotiwa na CNN inasema mwanamke huyo amenyongwa katika gereza la Tehrain, Iran ambapo alikuwa amefungwa baada ya kutenda kosa hilo mwaka 2007 wakati huo akiwa na umri wa miaka 19.
Mwanamke huyo amekutwa na hatia hiyo kutokana na kosa la kumuua aliyekuwa mfanyakazi wa wizara ya ulinzi na usalama nchini Iran, Morteza Abdolali.
Shirika la kimataifa la haki za binadamu Amnesty International limelaani kitendo cha Iran kutoa hukumu hiyo, ambapo mbali na jitihada ya kampeni mbali mbali zilizofanywa ikiwemo zile za kwenye mitandao ya kijamii katika kuipinga hukumu hiyo kuonekana kutozaa matunda.
Taarifa kutoka nchini humo zinasema mahakama ilitoa hukumu hiyo baada ya kutojiridhisha na utetezi alioutoa mahakamani kwamba alitenda kosa hilo akiwa anajilinda.
Utafiti wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2011 unaonesha Iran ni moja ya nchi zinazoongoza kwa ukiukwaji wa haki za binadamu ambapo nchi hiyo ina wastani wa kutoa hukumu ya kunyongwa mtu 1 kila baada ya masaa 8.

Related Posts:

  • Bangi halali kwa matibabu Jamaica    Baraza la mawaziri la Jamaica, limeidhinisha mswada ambao unahalalisha watu kumiliki kiwango kidogo cha Marijuana. Ina maana kwamba hii ni mara ya kwanza kwa jamii ya 'Warastafarian' wanaotumia Bangi kwa sa… Read More
  • CAF: Club kujigharamia Malazi   Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limefanyia marekebisho kanuni zake za michuano ya ngazi ya klabu kwa upande wa malazi ambapo sasa timu zitachagua na kujilipia zenyewe hoteli zinapokuwa kwenye mechi za u… Read More
  • Official HD Music Video-Y-Tony ft Barnaba - Mama Msanii wa bongo fleva anaekuja kwa kasi katika soko la muziki wa bongo,mwenye hit song ya masebene,ameachia video yake mpya aliyo mshirikisha Barnaba nyimbo inaitwa Mama Utengenezwaji wa video hii ulianza mwaka jana… Read More
  • WhatsApp yawabana watumiaji Mtandao wa WjhatsApp Mtandao wa kijamii wa What… Read More
  • Tunda man "Rais wa Tanzania ni Lowassa tu"    Mwana muziki toka katika kundi la Tip Top Connection la Manzese Tunda man, anasema kwa sasa Tanzania inahitaji kiongozi anayeweza kuendana na wakati wa sasa.   Akizungumza na Ubalozini.blogspot.co… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE