November 13, 2014

Baba mdogo wa marehem Geez Mabovu (30)  amesema kuwa Mbovu ambae amefikwa na mauti jana usiku majira ya sa mbili na dakika 15 alikuwa anasumbuliwa na kifua na kufariki akiwa nyumbani kwao
"Mimi naitwa Abasi Upete ni baba yake mdogo na Geez Mabovu, actually katikati hapa madaktari kifua kilikuwa kinamsumbua kwahiyo walikuwa wanashindwa kujua tatizo ni nini, maana amefia nyumbani tu kwahiyo wakasema hawawezi kufanya chochote mpaka waweze kupata makohozi ili tuweze kujuwa kifua kulikuwa kinamsumbua hasa ni nini kama ni kifia kikuu au tatizo gani lakini bahati mbaya ndio amefariki saa mbili na dakika kumi na tano. ni kama wiki mbili na nusu zilizopita hivi hali ilizidi kuwa mbaya katikati hapa lakini kaka yangu ambae ni baba yake alienda kumchukua Daresalaam kama wiki mbili na nusu hivi, tutakuwepo mlandege karibu na tenki la maji, ana miaka 30, mpaka sasa hivi hatujapata taarifa zozote unajua vijana hao, na mazishi yatakuwepo  saa kumi tutasalia katika msikiti wa mwangata maeneo ya mololo" amesema baba yake mdogo

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE