
Marekani imelaani kile ilichokitaja kuwa mipango
ya jeshi nchini Burkina Faso ya kulazimisha inachotaka kwa watu raia kufuatia kujiuzulu kwa rais wa nchi hiyo Blaise Compaore.
Jeshi limemteua kanali Isaac Zida kama kiongozi mpya wa serikali ya mpito.
Lakini
kwa upande wake Marekani inataka kuwepo utawala wa kiraia nchini
Burkina Faso mbali na mipango ya kuwepo kwa uchaguzi wa urais, wito
ambao pia ulitolewa na muungano wa Afrika.
Upinzani
nchini Burkina Faso unasema kuwa hautakubali uongozi wa kijeshi na
umeitisha maandamano leo Jumapili Bwana Compaore ameikimbilia Ivory
Coast baada ya kulazimishwa kuondoka madarakani kupitia maandamano.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment